- Madam Caroline alizungumzia madai yaliyozingira kifo cha kusikitisha cha mwanafunzi aliyejulikana kama Moses Nyang’au katika Shule ya Moi Comprehensive mjini Nakuru
- Wazazi waliandamana nje ya shule wakitaka majibu kufuatia kifo cha kutatanisha cha mtoto huyo wa darasa la nane wakati akisubiri kuhojiwa na mwalimu
- Imebainika mwanapatholojia alisema chanzo cha kifo cha Moses kilitokana na mzunguko mbaya wa damu mwilini, na sababu za hali hiyo pia zimebainika
Nakuru, Kenya: Madam Caroline amejitokeza kujibu tuhuma zilizotolewa dhidi ya Moi Comprehensive School kufuatia kifo cha mwanafunzi wa Darasa la Nane, Moses Nyang’au.

Source: Youtube
Maandamano ya wazazi shuleni
Baada ya kifo cha Moses, wazazi walikusanyika nje ya shule wakipinga tukio hilo walilolitaja kuwa la kutatanisha.
Polisi walilazimika kuingilia kati kutuliza hali, huku wazazi wakishinikiza majibu na kusukuma mwili wa mwanafunzi huyo kwa toroli la chuma kuelekea shuleni.
Tukio hilo lilitokea Jumatatu, Februari 23. Ilibainika kuwa shule ilijaribu kumpeleka mwanafunzi hospitalini, lakini juhudi hizo hazikufaulu kwani tayari alikuwa ameaga dunia.

Source: Youtube
Madam Caroline alisema nini?
Akizungumza na wanahabari, Madam Caroline alieleza kuwa mwalimu aliyetambuliwa kama Madam Abigael aliwaona wanafunzi wakiwa nje ya darasa, akawaagiza wasimame mbele ya darasa na kuanza kuwauliza maswali. Kabla hata hajamfikia Moses, mwanafunzi huyo alianguka.
“Kifo kilithibitishwa shuleni saa 4:10 asubuhi (10:10am). Hili ni tukio la huzuni kubwa kwa shule na tunaomba radhi kwa familia kwa yaliyotokea,” alisema.
Aliongeza kuwa mwalimu alimpeleka Moses kwa muuguzi wa shule, lakini hakuwapo wakati huo. Naibu mwalimu mkuu aligundua kuwa mwanafunzi huyo alikuwa anahangaika kupumua, ndipo Madam Abigael akamjulisha Caroline.
Caroline alisema alimchukua kwa gari lake binafsi na kuanza hatua za dharura. Walijaribu kuwasiliana na wazazi wake; baba hakupatikana kwa simu mara moja, hivyo wakaenda kumtafuta. Inasemekana baba huyo ni msambazaji wa sukuma wiki shuleni hapo.
Kwa mujibu wa Caroline, kabla madaktari hawajaanza uchunguzi wa kina, waliwataka wazazi waende kituo cha polisi kupata OB (Occurrence Book), jambo lililosababisha mchakato kuchelewa hadi saa sita mchana.

Pia soma
Familia Ambayo Lexus Yao ya KSh 35m Iliharibiwa Yasema Wavamizi Waliwatilia Dawa ya Usingizi
Ripoti ya daktari wa maiti ilisema nini?
Daktari wa maiti alihitimisha kuwa Moses alifariki kutokana na mzunguko duni wa damu mwilini.
Kulingana na daktari, hali hiyo inaweza kusababishwa na hofu kali au mabadiliko ya ghafla ya mpigo wa moyo.
“Tusingetaka kamwe kumdhuru mtoto huyo,” Caroline alisisitiza.
Wakenya walizungumziaje hotuba ya mwalimu mkuu?
Kauli ya Madam Caroline ilizua mjadala mitandaoni. Baadhi ya maoni ni:
- William Waweru Gikunju: Alisema wanafunzi walikuwepo wakati mtoto akianguka, swali ni wako wapi na kwa nini hawajasikika?”
- Mamake Sam: Alishangaa maswali kuhusu muda halisi wa kifo, muda ambao mama aliarifiwa, na hali ya mtoto alipofikishwa hospitalini.
- Fanice Ochieng-Okutah: Alitoa pole kwa mwalimu Abigael, akisema huenda anapitia mshtuko wa kiakili.
- Babake Sandra: Alisema ukweli huenda uko kwenye mchakato wa kuwauliza wanafunzi maswali mmoja mmoja.
- Wanyundi Lyzea: Alisema kazi ya ualimu ni ya hatari na inahitaji ulinzi wa Mungu, akibainisha kuwa walimu hubeba jukumu la mamia ya wanafunzi kila mwaka.

Pia soma
Nakuru: Wazazi Wavamia Shule na Maiti ya Mwanafunzi wa Gredi ya 8 Aliyefariki kwa Njia ya Ajabu
Kisa kingine: Kifo cha mwanafunzi Machakos
Katika tukio tofauti, polisi mjini Machakos wameanzisha uchunguzi baada ya mwanafunzi wa Kidato cha Nne kufariki dunia alipobanwa na boza la maji la shule.
Inasemekana wanafunzi waliitwa kusaidia kulisukuma baada ya kushindwa kuwaka, ndipo likamdondokea mmoja wao.
Wakili Ndegwa Njiru aliomboleza kifo hicho huku akieleza kilichotokea. Tukio hilo lilizua kilio cha umma kuhusu ongezeko la vifo vya wanafunzi katika shule za Kenya.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke
