Nchini DRC, mwezi mmoja baada ya kuondoka kwa waasi wa AFC-M23 kutoka Mji wa Uvira Kivu Kusini, makaburi ya halaiki yamegunduliwa wiki hii wakati huu ambapo familia nyingi hazina taarifa kuhusu vijana wao waliokamatwa wakati hao.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mashuhuda wanasema kati ya makaburi hayo ya halaiki, mawili yaligunduliwa karibu na kambi ya kijeshi iliyokaliwa na AFC/M23 kule Kavimvrira katika kitongoji cha Kilomoni yakuwa na miili zaidi ya mia moja.
Nyingine iligunduliwa ikiwa na takriban miili ishirini katika kitongoji cha Kilibula eneo la Kalundu, na miili karibu hamsini imegunduliwa katika kijiji cha Kabimba umbali wa kilomita nane kusini mwa mji wa Uvira. Paul ni mmoja wa wakazi wa kusini mwa Uvira, anashuhudia.
“Ilikuwa wakati wa vita, watu wengi walifariki. Tulikuta maiti ya watu huku na kule, ikiwa ni 10 au 20 walipelekwa nakwenda kuzikwa ndani ya shimu moja.” Alisema Paul.
Gavana wa jimbo la Kivu Kusini chini ya utawala wa Kinshasa, Profesa Jean-Jacques Purusi Sadiki, anathibitisha ugunduzi huu wa kutisha.
“Makaburi ya halaiki ambayo ndiyo kwanza tumeshagundua, la kwanza lipo katika eneo la Kavimvira lenye miili 132 na jingine liko Kilomita kadhaa karibu na mpaka na Burundi yenye miili 31.” Alisema Gavana wa Kivu Kusini.
Ghislain Kabamba ni mtetezi wa haki za binadamu Uvira.
“Imeonekana kwamba ni AFC/M23 walifanya hivyo na tunaomba viongozi wetu uchunguzi ufanyike ili miili hiyo itambulike na wale waliotenda uovu huo waadhibiwe kulingana na sheria.”
Licha ya ugunduzi huu, kundi la AFC/M23 halijasema lolote..