Juhudi za utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa zaidi ya wakimbizi Milioni Moja nchini Sudan Kusini zinakabiliwa na tishio kutokana na uhaba wa ufadhili katika idara muhimu zinazohusika na misaada kwenye Umoja wa Mataifa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Shirika la kuwahudumia waomba hifadhi (IOM), Sudan Kusini inasalia kuwa nchi ambayo ina idadi kubwa ya watu waliopoteza makazi yao duniani.

IOM inasema karibia watu Milioni 10 wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu ambapo mwaka huu peke yake Shirika hilo linakabiliwa na upungufu wa Dolla Milioni 29 katika mipango yake ya utoaji wa misaada kwa wakimbizi wa Sudan Kusini.

Mashirika ya kuwasaidia wakimbizi yamepunguza misaada yao kutokana na kukatika kwa ufadhili.
Mashirika ya kuwasaidia wakimbizi yamepunguza misaada yao kutokana na kukatika kwa ufadhili. AP – Florence Miettaux

Juba inaendelea kukabiliwa na changamoto ya idadi kubwa ya wakimbizi, wengi wao wakitokea katika nchi jirani ya Sudan. 

Tangu mwezi Februari mwaka wa 2023, zaidi ya watu Milioni 1 wamevuka mpaka na kuingia Sudan Kusini, asilimia 67 kati yao wakiwa ni raia wa Sudan Kusini wanaorejea kutoka Sudan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *