
Mjumbe maalum mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameteuliwa nchini Sudan. Tangazo hilo lilitolewa siku ya Jumatano. Raia huyo wa Finland, Pekka Haavisto, anamrithi Ramtane Lamamra wa Algeria, ambaye aliteuliwa mnamo mwezi Novemba 2023.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ramtane Lamamra alitaka kuondoka katika wadhifa wake baada ya juhudi zisizokoma za kujaribu kutuliza mgogoro nchini Sudan, bila mafanikio. Alishutumu uingiliaji kati wa nchi za kigeni kaika vita vinavyoendelea nchini Sudan, ambao alisema ulisumbua kazi yake. Uteuzi huu unakuja wakati vita vinakaribia kuingia mwaka wake wa nne, mwezi Aprili 2026.
Pekka Haavisto, mjumbe maalum mpya, kwa sasa ni mbunge wa Bunge la Finland na atachukua wadhifa wake mpya hivi karibuni. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika siasa na masuala ya kimataifa. Ameshikilia nyadhifa kadhaa za uwaziri katika serikali ya nchi yake, ikiwa ni pamoja na ile ya Waziri wa Mambo ya Nje. Pia ameshikilia nyadhifa za ngazi ya juu ndani ya Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN).
Mgogoro wa Sudan, unaochukuliwa kuwa mmoja wapo wa mizozo mikubwa zaidi duniani katika suala la misaada ya kibinadamu na usalama, si jambo la kawaida kwa mjumbe mpya. Kati ya mwaka 2005 na mwaka 2007, alihudumu kama Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya nchini Sudan. Alishiriki katika mazungumzo ya amani ya Darfur kama mshauri mkuu wa Umoja wa Mataifa. Kuanzia mwka 2009 hadi 2017, alihudumu kama Mwakilishi Maalum wa Finland wa Upatanishi na Usimamizi wa Migogoro barani Afrika. Pekka Haavisto pia amefanya kazi na Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, hasa Kosovo, Montenegro, Afghanistan, na Iraq.