
Tume ya kutoa msamaha nchini Uganda, imetoa ahueni kwa waasi wa zamani zaidi ya Elfu 28 na 340 tangu mwaka 2000, mwenyekiti wake akitoa wito kwa wale ambao bado hawajarejea nyumbani kufanya hivyo chini ya muda uliowekwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Akizungumza kwenye kikao na wanahabari Jumatano ya wiki hii, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Peter Onega, alisema walionufaika pakubwa na msamaha huo ni Pamoja na wapiganaji wa Kundi la LRA linaloongozwa na Joseph Kony.
Makundi mengine yaliyonufaika na mpango huu ni pamoja na lile linaloongozwa na Ali Bamuze pamoja na lile la kiislamu la ADF linalofanya shughuli zake Mashariki mwa DRC.
Jaji Onega, amesema juhudi zinafanyika kuwasiliana na viongozi wa makundi hayo waliohasi ili kuwasaidia kurejea nyumbani na kutangamana na jamii.
Hata hivyo, amesema kuna changamoto ya ucheleweshaji wa mchakato wa kuwajumuisha upya watakaonufaika, hali inayochangiwa na unyanyapaa katika baadhi ya maeneo, wanawake na watoto wakiathirika zaidi.