
Milipuko kadhaa imesikika mapema leo Alhamisi, Februari 26, 2026, katikati mwa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, kulingana na mwandishi wa habari wa AFP, kufuatia onyo kutoka kwa mamlaka kuhusu shambulio la Urusi, saa chache kabla ya mazungumzo ya Marekani na Ukraine huko Geneva yenye lengo la kukomesha vita.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Adui anashambulia jiji kwa ndege zisizo na rubani za kivita na makombora ya balestiki. Ulinzi wa angani unafanya kazi. Bakieni majumbani kwenu hadi tahadhari itakapoisha!” ameandika mkuu wa utawala wa kijeshi wa eneo hilo, Tymur Tkachenko, kwenye Telegram.
Mbali na mji mkuu wa Ukraine, miji mingine mikubwa imelengwa usiku kucha.
Kharkiv (kaskazini mashariki), jiji la pili lenye watu wengi zaidi nchini humo kabla ya uvamizi wa Urusi uliozinduliwa Februari 2022, limengwa na ndege zisizo na rubani na makombora, amesema meya wa jiji hilo, Igor Terekhov, ambaye pia ametaja milipuko kadhaa.
Mkutano umepangwa kufanyika Alhamisi huko Geneva
Katikati mwa Ukraine, huko Kryvyi Rig, mwanamume mwenye umri wa miaka 89 amejeruhiwa katika shambulio la Urusi lililoharibu jengo moja, kulingana na mkuu wa utawala wa eneo la Dnipropetrovsk, Oleksandr Ganja.
Hatimaye, huko Zaporizhzhia (kusini mashariki), “milipuko kadhaa” inayohusishwa na shambulio la Urusi imesikika, kulingana na Ivan Fedorov, mkuu wa utawala wa eneo hilo.
Wajumbe wa Ukraine na Marekani wanatarajiwa kukutana leo Alhamisi huko Geneva, Uswisi, kufanya kazi kwenye mazungumzo mapya ya pande tatu na Urusi ili kukomesha mzozo huo, ambao uliingia mwaka wake wa tano siku ya Jumanne.