
WAZIRI wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omar amewaagiza viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kuwa wabuni katika ukusanyaji wa mapato nchini. Akishiriki hafla ya futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar-es-salaam , Balozi Omar amesema serikali inampango wa kuendelea kuhamasisha makusanyo ya mapato katika maeneo mengine mikoani.
“ Hapa Dar-es-salaam inabidi kwa sasa tuache kidogo tumefanya sana hapa na sasa ni kwenda maeneo mengine Tanzania ili lengo la serikali liweze kutimia la ukusanyaji wa mapato kwa nchi nzima”, alisema Balozi Omar. SOMA: Naibu Waziri Fedha azindua boti ya TRA
Balozi Omar alikua na ziara ya kikazi ya siku mbili katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jijini Dar es Salaam, ambapo alikagua na kujionea utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na mamlaka hiyo hususan katika kukuza mapato ya Serikali kwa njia ya ukusanyaji wa kodi.