#HABARI: FBI imewafukuza kazi takriban maafisa 10, ambao wote walishiriki katika uchunguzi kuhusu jinsi Donald Trump alivyoshughulikia nyaraka za siri baada ya muhula wake wa kwanza.

Kusitishwa kwao kazi Jumatano, kumethibitishwa na CBS, na kulitangazwa muda mfupi baada ya mkurugenzi wa FBI, Kash Patel, kuiambia Reuters kwamba maafisa hao wa shirikisho walimchunguza alipokuwa raia wakati wa uchunguzi wa hati hizo.

Patel hakutoa ushahidi wowote wa makosa yaliyofanywa na wafanyakazi wa FBI waliofukuzwa kazi.

Baada ya Trump kuondoka Ikulu ya White House mwaka 2021, Wakili Maalum Jack Smith aliongoza uchunguzi dhidi ya Trump ambaye sasa ni Rais. Kesi moja ililenga kujua ikiwa Trump alijaribu kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa 2020.

Nyingine ilihusisha hati za siri ambazo Trump alizipeleka katika makazi yake ya Mar-a-Lago huko Florida na juhudi zake za kuzuia Wizara ya Sheria ya Marekani kuzipata.

Wafanyakazi wa FBI waliofutwa kazi Jumatano wote walishiriki katika kesi juu ya hati za siri.

Trump na washirika wake wawili walishtakiwa mwaka 2023, kufuatia uchunguzi wa Smith kuhusu hati hizo.

Wizara ya sheria pia imefungua mashtaka dhidi ya mkurugenzi wa zamani wa FBI James Comey, ambaye Trump alimfukuza kazi wakati wa muhula wake wa kwanza mwaka 2017, na Mwanasheria Mkuu wa New York Letitia James, ambaye aliongoza kesi dhidi ya Trump.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *