#HABARI: Kamati ya Uongozi wa Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), ikiongozwa na Mwenyekiti Dkt. Jim Yonazi, imekagua maendeleo ya mradi huo na kueleza kuridhishwa kwa hali ya juu na viwango vya ubora vilivyozingatiwa wakati wa utekelezaji.
Kamati imebainisha kuwa mradi huo umesimamiwa kwa ufanisi mkubwa unaoakisi thamani ya fedha za Serikali, huku ikisisitiza kuwa JNHPP imekuwa kielelezo cha mafanikio barani Afrika kwa kuleta unafuu wa nishati na kuimarisha gridi ya taifa.
Hadi kufikia Februari 2026, mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 na kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya nishati, ambapo uwezo wa uzalishaji umeongezeka kutoka megawati 1,600 mwaka 2021 hadi kufikia zaidi ya megawati 4,000 sasa.
Ongezeko hili la zaidi ya mara mbili limekuwa chachu ya ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii, likiimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika unaosambazwa katika maeneo mbalimbali nchini kupitia vituo muhimu kama kile cha Chalinze.
Aidha, juhudi za kuimarisha miundombinu ya usambazaji zinaendelea, ambapo ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze kwenda Dodoma umefikia asilimia 71.58 na ile ya kuelekea Mkuranga imefikia asilimia 59.76.
Kamati imehitimisha kwa kusema kuwa miradi hii ya kimkakati inaifanya Tanzania kuwa kitovu cha nishati na kivutio kikuu cha uwekezaji katika kanda ya Afrika Mashariki, Kati, na Kusini kutokana na nishati ya uhakika na endelevu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania