#HABARI: Kuelekea mchezo mkubwa wa Ligi Kuu ya NBC utakaofanyika siku ya Jumapili Machi 01, 2026 kati ya timu za Young Africans SC na Simba SC, katika Uwanja wa New Amaan Complex majira ya saa 02:15 usiku ambao pia unafanyika katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na mfungo wa Kwaresma, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama limesema limejipanga kikamilifu kuhakikisha kunakuwepo na ulinzi wa kutosha kabla, wakati na baada ya mchezo huo ili mashabiki wote waweze kushuhudia mechi hiyo kwa amani, utulivu na kuheshimu misingi ya imani zao.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi, mashabiki na wadau wa mpira wa miguu kuendelea kudumisha nidhamu, uvumilivu na mshikamano, sambamba na kuzingatia maadili ya vipindi hivi vitakatifu kwa kuepuka vitendo vya fujo, matusi, uchochezi au uvunjifu wa amani wa aina yoyote ndani na nje ya uwanja.
“Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka sheria.

Aidha, tunawasihi mashabiki kupanga ratiba zao mapema kwa kuzingatia muda wa ibada, futari na shughuli nyingine za kiimani, pamoja na kufika uwanjani kwa utaratibu ili kuepusha msongamano usio wa lazima. Vilevile madereva wa vyombo vya moto wanakumbushwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na maelekezo yatakayotolewa na askari waliopo kazini.”

Jeshi la Polisi linawahakikishia wananchi ulinzi wa kutosha na linawakaribisha wote kushuhudia mchezo huo kwa amani, upendo na kuheshimiana, ili kuendeleza sifa njema ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *