#HABARI: Mradi wa maji katika Kijiji cha Nyani, Kata ya Mafizi, umefikia asilimia 70 ya utekelezaji, jambo lililomfanya Mbunge wa Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, kuonyesha kuridhishwa na kasi ya mkandarasi wa mradi huo.

Mradi huo wa maji unaogharimu kiasi cha shilingi milioni 402.8 unahusisha ujenzi wa tanki la lita 50,000 na mtandao wa mabomba wa kilometa 16, ambapo Dkt. Jafo ameiomba Wizara ya Maji kutoa shilingi milioni 279.1 kwa ajili ya kazi zilizofanyika ili kukamilisha hatua zilizobaki kwa wakati.

Mbali na kumpongeza mkandarasi kwa uzalendo wake wa kufanya kazi kabla ya malipo, Dkt. Jafo amemsifu Meneja wa RUWASA Kisarawe, Mhandisi Evangelista Kahwili, kwa usimamizi makini wa miradi ya maji jimboni humo.

Kukamilika kwa mradi huu kunatarajiwa kuwa mkombozi kwa wananchi wa Nyani kwa kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kufuata maji, huku kukiimarisha afya na kuchochea shughuli za kiuchumi kijijini hapo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *