#HABARI: Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud amekagua miradi mitatu ya Idara ya Uhamiaji visiwani Zanzibar inayogharimu zaidi ya shilingi bilioni 25.

Miradi hiyo inajumuisha ujenzi wa ofisi ya Kamanda wa Mkoa Mjini Magharibi, Kituo cha Wilaya ya Kusini, na Chuo cha Uhamiaji.

​Akizungumza leo mara baada ya ukaguzi wa Miradi hiyo, Mhe. Ayoub amewataka wakandarasi kukamilisha kazi hizo kwa wakati, ambapo jengo la Mjini Magharibi na mradi wa Chuo sasa yanatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi 2026.

Ambapo amesisitiza kuwa Serikali haitafurahishwa na ucheleweshaji utakaozuia Askari kufanya kazi katika mazingira bora.

Akichanganua gharama za Mradi huo amesema kuwa mradi wa Mjini Magharibi unagharimu bilioni 9.9, kituo cha Kusini bilioni 3.1, na mradi wa chuo unagharimu bilioni 12. Fedha zote hizo zimetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

​Aidha, Naibu Waziri ameongeza kuwa maboresho hayo ya miundombinu ya Idara ya Uhamiaji yanakwenda sambamba na uimarishaji wa mifumo ya kidijitali katika kuhakikisha huduma za Kiuhamiaji zinatolewa kwa weledi na ufanisi mkubwa

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *