#HABARI: Serikali imetoa wito kwa wananchi waliokamilisha taratibu za mirathi na kupata haki zao kurejea mahakamani kufunga rasmi mashauri hayo ili kupunguza mlundikano wa kesi zinazoonekana bado ziko wazi.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab Katimba, amebainisha kuwa kutokufungwa kwa kesi hizo kunasababisha takwimu za mahakama kuonekana na mashauri mengi yasiyohitajika, huku akisisitiza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha sekta ya sheria kupitia TEHAMA na kuboresha miundombinu ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wakati.

Katika ziara yake kwenye Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke (IJC), Mhe. Katimba amepongeza mfumo huo unaounganisha ngazi mbalimbali za mahakama na kutoa huduma za kijamii kama ushauri nasaha na msaada wa kisheria katika eneo moja.

Amesema uanzishwaji wa vituo hivyo unalenga kusogeza huduma karibu na wananchi na kuzingatia mahitaji ya makundi maalum, ikiwemo uwepo wa vyumba vya kunyonyesha, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuhakikisha utoaji haki nchini unazingatia utu na usawa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *