#HABARI: Ziara ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba Jijini Arusha, imewazindua watendaji na kujikuta wakibaini ujenzi wa shule ya ghorofa usio na vibali na watoto kulazwa katika bweni wakati ujenzi ukiendelea kwenye ghorofa hizo.

Hayo yamebainika leo wakati Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude na Kamati ya Usalama ya Wilaya walipofanya ziara kwenye shule ya Nariva Hill na kufanya ukaguzi katika madarasa, mabweni, jikoni na eneo wanalojenga ghorofa juu ya bweni lililokuwa linatumika.

Katika ziara hiyo shuleni hapo ambayo ilikuwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu, viongozi hao walibaini kuwepo kwa msongamano wa wanafunzi wa kike wanaolala katika bweni la muda, ilhali hawana vyoo wala mabafu kwenye ghorofa yao. Pia walibaini baadhi ya watoto wanalala wawiliwawili kwenye kitanda kimoja.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *