Mjerumani Zemke Jermaine wa kampuni ya Rembe Rad-Net, hapo jana alifanikiwa kushinda hatua ya 5 ya mashindano ya Baiskeli ya Tour du Rwanda kuzunguka mji wa Rubavu, mbio zilizokuwa na umbali wa kilometa 82.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa imepewa jina la Rubavu Criterium, njia hiyo ilikuwa ya mizunguko tisa kando ya barabara zenye mandhari nzuri kando ya ziwa, ikiwa ni mara ya kwanza kwa jimbo hilo la magharibi mwa Rwanda kuandaa mbio za mzunguko wa Tour du Rwanda.

Zemke alitumia saa 1, dakika 44 na sekunde 27 kuwashinda Itamar Einhorn wa Israeli na Henok Mulueberhan wa Eritrea.

Waendesha baiskeli watatu bora walirekodi muda mmoja huku Moritz Kretschy wa Timu ya NSN Development akibakia na jezi ya njano licha ya kumaliza katika nafasi ya 31.

“Ilikuwa hatua fupi sana, lakini haikuwa rahisi. Lakini timu yetu ilifanikiwa kubaki mbele. Katika dakika za mwisho, nilijua ningeweza kufanya kitu,” Zemke mwenye umri wa miaka 20 aliliambia jarida la Michezo la Times.

Zikiwa zimesalia raundi tatu, Patrick Byukusenge wa Timu ya Rwanda alijaribu kuendesha kwa kasi baada ya kilometa 52, lakini hata hivyo hakuweza kufua dafu.

Mshindi wa Hatua ya Nne Jurgen Zomermaand alimaliza nje ya tano bora.

Eric Muhoza wa Timu ya Amani alikuwa mwendesha baiskeli pekee wa Rwanda aliyeshika nafasi ya kwanza, akimaliza katika nafasi ya 15, huku Moise Mugisha wa Benediction BanAfrica akishika nafasi ya 25.

Matokeo ya Jumla

1. Zemke Jermaine (Rembe Rad-Net) – 1h 44’27”

2. Itamar Einhorn (NSN Development Team) – same time

3. Henok Mulueberhan (Eritrea National Team) – same time

4. Even Yemane (Bike Aid) – same time

5. Hodei Gabina Munoz (Soudal Quick-Step Development Team) – same time

Today: Stage 6 from Rubavu to Musanze – Km 84.1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *