TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Februari 27, 2026 imekutana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir, kwa ajili ya kupata maoni na ushauri wake.

Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Lake Tanganyika uliopo katika Jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo, pande hizo zimejadili namna matukio ya uvunjifu wa amani yalivyoanza, athari zake kwa wananchi, mali na miundombinu pamoja na mapendekezo ya hatua za kuchukua ili matukio kama hayo yasijirudie. SOMA: Tume Yakutana Mwamunyange,Waitara

Hivi karibuni, Mamlaka ya Uteuzi imeiongezea Tume muda wa siku 42 kuanzia Februari 20, 2026 ili kukamilisha uchunguzi wake na kuwasilisha taarifa kabla au ifikapo Aprili 3, 2026. Kwa sasa Tume inaendelea kufanya mahojiano na wadau mbalimbali, wakiwemo waathirika wa matukio hayo, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupata suluhisho na kuimarisha amani nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *