
Mkuu wa tume ya haki ya Umoja wa Mataifa Volker Turk ameonya kuhusu kudodrora kwa hali nchini Sudan Kusini, huku akitoa wito wa hatua ya haraka kuchukuliwa kuzuia taifa hilo kutumbukia tena kwenye vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Turk amesema kuwa hatua za haraka zinahitajika ili kudumisha mkataba wa amani na kuzuia mgawanyiko unaoweza kuirejesha nchi hiyo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Vurugu zimeongezeka nchini humo katika wiki za hivi karibuni, ambapo takriban watu laki mbili na elfu 28 wameyakimbia makazi yao tangu mwezi Disemba katika jimbo la Jonglei.
Aidha Turk ameonya kuwa hali nchini humo iliripotiwa kudodora hata zaidi katika mwezi wa Januari, ambapo ukiukaji wa haki za binadamu uliongezeka kwa asilimia 45 ikilinganishwa na miezi iliotangulia.
Mbali na ukiukaji wa haki, Turk pia amelaani kukithiri kwa matukio ya unyanyasaji wa kingono, huku pia akielezea wasiwasi wake juu ya matamshi ya chuki na uchochezi wa ghasia vinavyoweza kuwa uhalifu wa kimataifa.