Katika hatua inayolenga kupunguza mvutano, Sierra Leone imesema kuwa Guinea jana iliwaachilia huru wanajeshi na maafisa wake wa polisi 16 waliokamatwa siku ya Jumanne.

“Maafisa wote wa usalama waliokamatwa na serikali ya Guinea wamekabidhiwa salama salimini kwa Sierra Leone,” imeeleza Wizara ya Habari katika mtandao wa kijamii.

Freetown imesema kuwa askari hao walikamatwa na wanajeshi wa Guinea walipokuwa wakijenga kituo cha mpakani na kingine katika mji wa mpakani wa Kaliyereh.

Guinea, kwa upande wake, imesema kuwa wanajeshi kadhaa wa Sierra Leone waliokuwa na silaha waliingia katika eneo lake bila kibali, na kuwatia mbaroni na askari wake wa usalama.

Waziri Mkuu wa Guinea Conakry, Amadou Oury Bah, aliahidi juzi Alhamisi kwamba mzozo huo utasuluhishwa haraka kupitia diplomasia.

Nchi hizo mbili zina mpaka wa pamoja wa kilomita 700 na ziliwahi kuathiriwa na mizozo katika kipindi cha vita vya ndani vya Siera Leone vilivyoendelea kwa zaidi ya muongo mmoja na kumalizika mwaka 2002.

Nchi hizo mbili zina mpaka wa pamoja wa kilomita 700 na ziliwahi kuwathiriwa na mizozo katika kipindi cha vita vya ndani vya Siera Leone vilivyodumu kwa zaidi ya muongo mmoja na kumalizika mwaka 2002.

Tukio hili limejiri  katika eneo ambalo limekuwa likizozaniwa kati ya nchi mbili hizo kwa zaidi ya miaka 20, huku Sierra Leone ikidai kuwa ni mali yake, na Guinea ikiwa imetuma wanajeshi katika eneo hilo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *