Marekani na Israel, zimetekeleza mashambulio ya kijeshi nchini Iran siku ya Jumamosi, ikimlenga kiongozi wa kiroho Ayatollah Ali Khamenei na rais Masoud Pezeshkian, huku Tehran ikilipiza kisasi kwa kurusha makombora katika nchi za eneo la Ghuba, ikiwemo Israeli.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mashambulio hayo yamejibiwa na Iran, ambayo imerusha makombora yake nchini Israel na kulenga kambi za jeshi la Marekani katika nchi za Bahrain, Qatar, Falme za Kiarabu na Kuwait.
Jeshi la Iran linasema, litaendelea na mashambulizi kulenga kambi za jeshi la Marekani, katika eneo la Ghuba, kwa kile inachosema, hadi adui ambaye ni Marekani na Israeli, watakaposhindwa.
Nchini Iran, shambulio katika shule moja lilitokelezwa na Israeli, limesababisha vifo vya watu 40, huku Falme ya Kiarabu ikisema mtu mmoja ameuawa kufuatia shambulio ya Iran.
Urusi imelaani mashambulio ya Marekani na Israeli nchini Iran, ikisema ni kitendo hatari, kunachoweza kusababisha vita vya kikanda, na kuwataka raia wake kuondoka Iran na Israeli haraka.
Naye rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ametaka kufanyika kwa dharura kwa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kujadili mzozo huu.
Hatua hii ya Israel na Marekani imekuja, wakati wajumbe kutoka Washington na Tehran, wakikutana jijini Geneva, kujadili uwezekano wa kupatikana kwa mkataba wa kidiplomasia kuhusu mradi wa nyuklia wa Iran, ambao Marekani na Israeli zinasema, nchi hiyo inatengeneza silaha za maangamizi.