.

Muda wa kusoma: Dakika 1

Israel imeanzisha kile ilichokiita “shambulio la tahadhari” dhidi ya Iran.

Katika taarifa yake asubuhi ya leo, Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz ametangaza “hali maalum na ya dharura” kote Israel.

Milipuko mitatu imesikika katikati mwa jiji la Tehran, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran.

Shirika la Habari la Fars linasema kuwa limepokea taarifa kwamba makombora kadhaa yamepiga eneo mji mkuu wa Iran.

Taarifa zaidi za milipuko mjini Tehran sasa zinaibuka katika vyombo vya habari vya Iran.

Shirika la habari la Fars linaloshirikiana na serikali nchini Iran linaripoti kuwa milipuko mingine ilisikika kaskazini na mashariki mwa Tehran.

Endelea kuwa nasi kwa maelezo zaidi kadiri tutakavyozipokea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *