
Milipuko yaripotiwa jijini Tehran, Israel ikitangaza kuwa imetekeleza shambulio la kombora nchini Iran.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na Shirika la Habari la The Associated Press, shambulio hilo limetokea karibu na Ofisi za kiongozi wa wa juu wa Kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.
Naye Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz amesema nchi yake imetekeleza shambulio hilo kama njia moja ya kuondoa kile amekitaja kama tishio kwa nchi yao.
Nalo jeshi la Israel limewataka raia kuchukua tahadhari kutokana na uwezekano kuwa Iran inaweza kurusha makombora kuelekea Israel, milio ya vingora ikikisika jijini Jerusalem.
Tayari mamlaka ya viwanja vya ndege nchini Israel imetangaza kuwa imefunga anga yake kwa ndege za abiria wa kiraia, ikiwataka raia wasije kwenye viwanja vya ndege.