Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezitolea wito nchi mbalimbali kupinga simulizi zinazochochewa na hofu kuhusu suala la uhamiaji, akisisitiza kwamba “uhamiaji si mgogoro”.

Antonio Guterres amehimiza ushirikiano madhubuti kimataifa ili kushughulikia suala la uhamiaji.

Uhamaji wa binadamu unaunda ulimwengu wetu kwa kiasi kikubwa,” Guterres amebainisha haya wakati wa hotuba yake kwa Baraza Kuu la UN katika ripoti yake kuhusu Mkataba wa Kimataifa wa Uhamiaji Salama, Ulioratibiwa na wa Kawaida.

Guterres amesisitiza kuwa wahamiaji si wahalifu. Ni waathirika na kwamba “wahalifu halisi ni mitandao isiyo na huruma inayojihusisha na magendo na biashara haramu.”

Amesema mitandao hiyo inanufaika kutokana na wahamiaji waliokata na pia kukosekana njia mbadala zilizo salama. “Mitandao hiyo inapasa kufuatiliwa na kufikishwa mahakamani.

Amesema ili kupatia ufumbuzi suala hili, njia za wazi za uhamiaji wa mara kwa mara zinapasa kurahisishwa nakupanuliwa, na ushirikiano wa kimaendeleo unapasa kuwepo ili kuweka kikamilifu katika elimu, ujuzi na uandaaji wa ajira zenye staha katika nchi asilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *