
Marekani na Israel zimeanzisha mashambulio kuelekea katika Miji mbalimbali likiweo jijini kuu la Tehran nchini Iran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mashambulio haya yanajiri baada ya Rais wa marekani Donald Trump kueleza kusikistishwa na hatua ya Iran kuonekana kukwamisha mazungumzo kuhusu silaha zake za nyukilia.
Kwa mujibu wa Rais Trump, lengo la Marekani kuishambulia Iran ni kuondoa kile anasema ni tishio kutoka kwa nchi hiyo ya Kiisilamu.
Naye Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz ametaja mashambulio hayo kama yakujilinda.
“Marekani imeanzisha oparesheni kubwa ya kijeshi nchini Iran”, Rais Trump amesema kupitia mkanda wa video kwenye mitandao yake ya kijamii.
“Tunaenda kuharibu makombora yote pamoja na kusambaratisha viwanda vyao vya kujenga silaha. Tutamaliza kabisa jeshi lao la majini,” amesema Trump.
Licha ya mashambulio hayo, Vyombo vya habari vya Iran vimethibitisha kuwa Rais Pezeshkian yupo salama.