ZIKIWA zimesalia saa chache ipigwe mechi ya Dabi ya Kariakoo kwenye Uwanja wa New Amaan Complex hapa Unguja, kikosi cha Yanga leo Februari 28, 2026 kimefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo, huku mchezaji nyota wa timu hiyo, Pacome Zouzoua akionekana kufanya mazoezi peke yake.

Pacome aliripotiwa kuwa kwenye matibabu ya majeraha aliyoyapata na kwamba hali yake ya kiafya haijawa sawa kwa asilimia mia.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara, itachezwa kesho Jumapili Machi 1, 2026 kuanzia saa 2:15 usiku.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Gocanlves amesema hana uhakika wa kumtumia nyota huyo kwenye mchezo wa kesho kwani hajapona kwa asilimia zote.

Mechi ya mwisho Dabi ya Kariakoo katika Ngao ya Jamii, Pacome ndiye aliyefunga bao na kuipa Yanga ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *