Ayatollah Ali Khamenei adjusts his glasses in a 2024 photograph. He is wearing a black head covering and brown robe. He has a long grey beard which reaches from his chin to his head.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maoni na sera kali za mamlaka za Ayatollah Ali Khamenei zimekuwa na mchango mkubwa nchini Iran kwa karibu miongo minne.

Khamenei, 86, amekuwa kiongozi wa pili mkuu tangu mapinduzi ya 1979 baada ya kifo cha Ruhollah Khomeini mnamo mwaka 1989 na mwenye mamlaka ya juu zaidi nchini humo.

Kama kiongozi mkuu, alikuwa akidhibiti siasa za nchi, jeshi na taasisi za kidini za Iran ikiwa ni pamoja na kutoa mwongozo wa uhusiano wa masuala ya kigeni.

Kabla ya kuchukua wadhifa huo alikua rais wa taifa hilo kwa mihula miwili kuanzia 1981 hadi 1989.

Mamlaka ya ofisi yake yamemfanya Khamenei kuwa na nguvu zote kama mkuu wa nchi na kamanda mkuu wa jeshi, ikiwa ni pamoja na kikosi cha Revolutionary Guards.

An Iranian woman poses with a portrait of Supreme Leader Ayatollah Ali Khamenei. It is a sunny day, with blue skies. People wearing coats are gathered in the background and placards are laid in a pile on the ground.

Chanzo cha picha, Getty Images

Malezi ya kidini

Ali Khamenei alizaliwa Mashhad, jiji la pili kwa ukubwa nchini Iran, mwaka wa 1939.

Baba yake alikuwa kiongozi wa kidini wa Shia, tawi kuu la Kiislamu la Iran.

Khamenei alizungumzia sana utoto wake kama “maskini lakini mcha Mungu”, akisema mara kwa mara hakula chochote ila “mkate na zabibu”.

Alianza masomo ya dini huko Mashhad, akakaa kwa muda mfupi huko Najaf, Iraqi, kisha akasoma katika chuo cha dini katika mji wa Qom nchini Iran.

Wanachuoni kadhaa walimfundisha, ikiwa ni pamoja na Khomeini, ambaye baadaye alianzisha Jamhuri ya Kiislamu.

Khamenei kneeling while praying in front of a green curtain with a photograph of Khomeini leaning against it, on 31 January 2026, ahead of the 47th anniversary of the 1979 revolution. The photo is taken through metal railings that are out of focus in the foreground.

Chanzo cha picha, Office of the Supreme Leader via EPA

Khamenei alijiunga na wakosoaji wa Shah wa Iran, mfalme ambaye hatimaye alipinduliwa na mapinduzi ya mwaka 1979, ambayo mara nyingi hujulikana kama Mapinduzi ya Kiislamu.

Kwa miaka mingi, Khamenei aliishi kwa kujificha au alifungwa gerezani.

Polisi wa siri wa Shah walimkamata mara sita, na alikabiliwa na mateso.

Khamenei sits cross-legged on a rug surrounded by men who are also sitting on rugs. Other people are standing behind them.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati wa mapinduzi, Khamenei hakuwa mtu maarufu kati ya watu waliokuwa karibu na Ayatollah Khomeini, lakini alijulikana haraka baada ya ghasia hizo.

Alijiunga na Baraza la Mapinduzi lililoongoza mapinduzi, na kuwa baraza la uongozi la muda baada ya kuanguka kwa utawala wa Shah.

Jukumu lake la kwanza la serikali ya Jamhuri ya Kiislamu lilikuwa naibu wa Wizara ya Ulinzi.

Khomeini alimteua kuwa kiongozi wa Sala ya Ijumaa huko Tehran mwaka huo, cheo ambacho alikishikilia rasmi kwa muda mrefu.

Mahubiri ya kisiasa ya Ali Khamenei, yaliyotangazwa nchi nzima, yalimfanya ajulikane ndani ya uongozi mpya.

Jaribio la mauaji

Khamenei lying in a hospital bed with a raised back. His right hand is bandaged. A light sheet covers his legs and waist.

Chanzo cha picha, ​​Khamenei.ir

Mnamo mwaka 1981 Juni, Khamenei alinusurika jaribio la mauaji.

Kundi la wapinzani lililipua bomu kwenye mhadhara wake.

Huenda shambulizi hilo liliokoa maisha yake.

Khamenei alikuwa mwanzilishi mwenza na hatimaye kiongozi wa chama cha Islamic Republican, ambacho kilisaidia uongozi wa baada ya mapinduzi kuimarisha mamlaka.

Hata hivyo, alikuwa hospitalini wakati wa shambulizi kubwa la mabomu katika makao makuu ya chama hicho.

Mapafu yake yalichukua miezi kadhaa kupona kutokana na shambulio hilo ambalo lilifanya mkono wake wa kulia kulemaa kabisa.

Baadaye mwaka huo huo, akawa mgombea wa urais wa Iran.

Ali Khamenei standing in front of three microphones as he addresses the Assembly of Experts. His left hand is raised as he gestures. Behind him is a large panel with the heads of delegates visible as they sit on the row behind him.

Ayatollah Khomeini alilidhibiti baraza lililoamua nani angesimama, na Ali Khamenei alishinda kwa 97% ya kura.

Hotuba ya kuapishwa ya Khamenei ilikuwa mwongozo wa urais wake, ukishutumu “mkengeuko, uliberali, na wafuasi wa mrengo wa kushoto waliopendelea Marekani”.

Vita vya Iran-Iraq

Nchi jirani ya Iraq iliivamia Iran miezi kadhaa kabla ya uchaguzi.

Rais wa Iraq, Saddam Hussein, alihofia mapinduzi ya Iran yangedhoofisha utawala wake.

Kabla ya kuwa rais, mwanzoni mwa vita Khamenei alitumia miezi kadhaa vitani.

Katika miaka minane ya vita, mamia ya maelfu walipoteza maisha pande zote mbili.

An October 1980 image of Iraqi artillery shelling Abadan and Khorramshahr, in Iran, during the Iran-Iraq war. A gun on wheels about 5 times as tall as a soldier is smoking, having just been fired. Five men are standing behind it. Two have their hands in the air. One is bent and is tugging on a cable connected to the gun.

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika kipindi cha mzozo huo, Iraq ilitumia silaha za kemikali dhidi ya vijiji vya mpakani vya Iran na kushambulia miji ya mbali ikiwemo Tehran kwa makombora.

Vita hivyo vilifanya Khamenei kuendelea kutoiamini Marekani, ambayo iliunga mkono Iraq.

Ali Khamenie walking past a line of Chinese soldiers standing to attention while a military official in green uniform walks behind him. Khamenie is wearing a black head covering, brown tunic and grey shirt. He has a grey beard and darkened glasses.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiongozi Mkuu

Mnamo mwaka 1989, Ayatollah Khomeini alikufa, na Baraza la Wataalamu wa Uongozi likamchagua Khamenei kuwa mrithi wake.

Kiongozi huyu mkuu mpya alionekana na wengine kuwa na rekodi dhaifu katika masomo ya kidini.

Ayatollah Khamenei making a speech in 1986. He is wearing a black robe with grey shirt and black head covering. His fists are in the air.

Chanzo cha picha, Getty Images

“Mimi ni mtu mwenye makosa na mapungufu mengi, na kwa kweli ni mwalimu wa kidini mwenye elimu kidogo sana,” alikiri katika hotuba yake ya kwanza ofisini.

“Hata hivyo, nimepewa jukumu na nitatumia uwezo wangu wote na imani yangu yote kwa Mwenyezi kuweza kubeba jukumu hili zito.”

Gaddafi , sitting to the right of the image, looks at Khamenei as the Iranian leader talks. Gaddafi is holding his hands together on his lap. He is wearing a white robe with golden embroidery on the sides, a black jacket and dark red shirt with no collar, buttoned to the top. Khamenei is holding his hand up as he speaks. He is wearing black clothing on his head, a grey and black jacket and cream shirt. The pair are sitting next to each other on a sofa, with desk chairs and a meeting table behind them.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa kukosa heshima kwa viongozi wakuu wa kidini na umaarufu wa Khomeini, Khamenei aliishi kwa tahadhari.

Lakini baadaye alianzisha mitandao ya waliomtii katika mahakama, polisi, vyombo vya habari, viongozi wa kidini, bunge, kikosi cha Revolutionary Guards na vyombo vya kijasusi.

Karim Sadjadpour, mwenzake katika Shirika la Carnegie kwa ajili ya Amani ya Kimataifa mjini Washington, aliiambia BBC News kwamba uwezo wa Khamenei unategemea “kundi lililoshikamana la viongozi wa kidini wenye msimamo mkali na vikosi vya Ulinzi vya Revolutionary”.

Vyombo vya habari vya serikali ya Irani vilimuonyesha kama aliyeishi kwa shida huko Tehran na mke wake, watoto na wajukuu.

Ayatollah Khamenei shown on a white-cloth banner with Persian writing drawn on it. Cameras with video screens are pointed towards the banner.

Chanzo cha picha, Getty Images

Alizuia maandamano

Hadi kifo chake, Khamenei ameshutumiwa kikandamiza upinzani.

Mnamo mwaka 1999, alisitisha maandamano ya wanafunzi.

Muongo mmoja baadaye, walioandamana kupinga uchaguzi wakidai kuwa uliibiwa walinyunyiziwa pilipili, kupigwa na kufyatuliwa risasi.

A wide city street packed with thousands of male and female protests on 15 June 2009. Some people are holding green flags, while others are holding posters. Tall buildings are on either side and a metal bridge is in the background.

Chanzo cha picha, AFP

Mnamo mwaka wa 2019, kuongezeka kwa bei ya mafuta kulisababisha maandamano ya barabarani, na mamlaka ikaminya mtandao.

Shirika la Amnesty International linasema polisi waliwafyatulia risasi waandamanaji hadi kufa.

Wanawake wanaofanya kampeni dhidi ya uvaaji hijab waliteswa na kuwekwa katika kizuizi cha faragha.

Mwanasheria mmoja wa kike wa haki za binadamu alihukumiwa kifungo cha miaka 38 jela na kuchapwa viboko 148.

Mnamo mwaka 2022, alikumbana na changamoto kubwa kufuatia kifo cha Mahsa Amini akiwa chini ya ulinzi – mwanamke wa Kikurdi mwenye umri wa miaka 22 alikamatwa kwa kukataa kuvaa hijabu.

Shirika la Habari la Wanaharakati wa Kutetea Haki za Kibinadamu la Iran (HRANA) lenye makao yake makuu nchini Marekani limesema lilipokea majina ya zaidi ya watu 400 waliouawa katika maandamano yaliyofuata.

A wide street in Tehran blocked by vehicles, including cars and motorcycles, during the daytime on 21 September 2022. Dozens of people are gathered in front of and among the vehicles. A blur imposed by the BBC conceals the identities of people in the lower part of the image and nobody can be identified in the shot. A fire is burning in the background, with flames and dark black smoke billowing into the air. Green trees line both sides of the street. Tall buildings are in the background.

Chanzo cha picha, EPA

Katika msimu wa baridi wa 2025-26, kulitokea mfululizo wa maandamano ya mitaani nchini Iran, yaliyosababishwa na kuzorota kwa uchumi.

Mamlaka zilianzisha kamata kamata ya watu. Khamenei alikiri kuwa maelfu ya watu waliuawa, lakini aliwashutumu maadui kwa kuandaa ghasia.

“Wale wanaohusishwa na Israel na Marekani walisababisha uharibifu mkubwa na kuua maelfu ya watu kadhaa,” alisema na kuongeza kuwa walichochea machafuko. “Walifanya uhalifu na kosa kubwa,” Khamenei alisema.

A view from a balcony at night of a street filled with people, stretching into the distance, marching towards the camera on 8 January 2026. The road is lit by streetlights, car headlights and lights from buildings. To the left is a balcony where people are watching. A woman nearby is clapping.

Chanzo cha picha, User generated content

Shirika la HRANA limesema serikali ilivyojibu ilijumuisha “utumiaji nguvu kwa kukusudia kuua”.

Iliripoti kwamba zaidi ya watu 7,000 waliuawa, wengi wao wakiwa waandamanaji, na zaidi ya watu 200 kati ya wale waliokufa walikuwa “wajeshi na vikosi vya serikali”.

Marufuku ya chanjo ya Corona

Uchunguzi wa mwaka 2022 uliofanywa na BBC News Persian ulikadiria kuwa ugonjwa wa corona uliua watu 300,000 nchini Iran wakati wa janga hilo – zaidi ya mara mbili ya idadi rasmi ya vifo wakati huo.

A male hospital employee wearing a protective blue suit and white face mask checks the body of a medical member of staff who died from Covid. This is taking place inside a morgue in Rasoul-e-Akram hospital in western Tehran on 8 December 2020. The body is in a black bag that is placed inside an open rack. Another body is in a similar bag in the compartment next to where the worker is checking the body.

Chanzo cha picha, NurPhoto / Getty Images

Bila kutoa ushahidi, Khamenei alidai, “Inasemekana kwamba sehemu moja ya virusi hivi imeundwa mahsusi kwa ajili ya Iran, kwa kutumia maarifa ya maumbile ya Kiirani”.

Wakati usambazaji wa chanjo ulimwenguni ulipoanza – ukiongozwa na kampuni za dawa za Marekani na Ulaya – alipiga marufuku uagizaji wa chanjo za Marekani na Uingereza.

Ripoti za baadaye zilisema yeye binafsi alidungwa moja ya chanjo kadhaa zilizotengenezwa na Irani.

Khamenei waves to a crowd by standing up in an open-topped car on 18 September 1998 in Tehran. Several thousand Iranians took to the streets to express anger at the Taliban in Afghanistan ahead of a funeral for a group of Iranians killed by the militant group.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Kupinga Marekani

Muda mfupi baada ya mapinduzi ya mwaka 1979, wanafunzi wa chuo kikuu watiifu kwa Khomeini waliukalia ubalozi wa Marekani, wakiwachukua mateka wanadiplomasia na wafanyakazi katika maandamano ya Marekani.

Utekaji nyara huo ulidumu kwa siku 444 na ulisaidia kuweka msimamo dhidi ya Marekani na Magharibi kama sera rasmi ya serikali.

Blindfolded people stand in a group. Their blindfolds are white and tied around their heads. They are wearing Western-style trousers and shirts. Most of the group are men, and it is unclear from the clarity of the black-and-white image if some are them are women.

Chanzo cha picha, Getty Images

Baada ya mashambulizi ya Septemba 11 nchini Marekani, Rais Bush aliitaja Iran katika kile alichodai ni ‘Taifa lenye kufadhili ugaidi’.

Iran iliunga mkono Hezbollah – kundi la Shia lenye silaha huko Lebanon – kama mshirika wake katika mzozo ambao umesalia kidogo tu uendelee na kuwa wa kudumu na Israeli.

Khamenei aliikosoa Marekani, lakini sera zake hazikuidhinisha wala kuzikabili Marekani moja kwa moja.

Mpango wa Nyuklia

Khamenei views a model of a nuclear facility, in Tehran on 11 June 2023. He is wearing a blue face mask and traditional clothes while other men stand around him. One is wearing a white laboratory jacket. The model is in a display cabinet and consists of a white reactor dome and other buildings in one location, along with the framework of a rectangular building with models of people in it nearby.

Chanzo cha picha, Office of Iranian Supreme Leader / WANA via Reuters

Khamenei alizitaja silaha za nyuklia kuwa si za Kiislamu na mwaka 2003 alitoa fatwa (tafsiri ya sheria za Kiislamu) dhidi ya kuzitengeneza.

Hata hivyo, Israel na nchi za Magharibi ziliamini kwamba, wakati Mahmoud Ahmadinejad alikuwa rais, Iran ilikuwa na nishati ya nyuklia na mipango ya kisasa ya makombora kama kitu cha kuficha uwezo wa silaha za nyuklia.

Vikwazo vilivyofuata vilifanya Iran kuwa nchi masikini.

Khamenei looking downwards at Ahmadinejad, who is talking and appearing to be partially smiling. Khamenei is wearing a traditional black robe and black head covering. Ahmadinejad has a black open-necked shirt, a light grey jacket and no head covering. He has a thin grey beard and black hair that is partially grey.

Chanzo cha picha, Khamenei.ir

Mnamo mwaka wa 2015, Iran, Marekani, Uingereza, Ufaransa, Uchina, Urusi na Ujerumani zilifikia makubaliano ya kuzuia urutubishaji wa madini ya Urani nchini Iran.

Hata hivyo, Donald Trump alijiondoa wakati wa urais wake wa kwanza wa Marekani akiuita mkataba huo “uongo mkubwa kwamba utawala wa mauaji ulitamani mpango wa amani wa nishati ya nyuklia.”

Iran ilisisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia ulikuwa wa amani, na kwamba Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki limethibitisha ushirikiano wake.

Rais wa zamani wa Marekani Barrack Obama, ambaye alitia saini mkataba huo, aliandika mkataba huo “unafanya kazi”.

Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zilisema “zinajutia” uamuzi wa Marekani.

Wakati urais wa kwanza wa Trump ukikaribia, Marekani ilimuua afisa mkuu wa kikosi cha Revolutionary Guard Qasem Soleimani. Khamenei aliapa kulipiza kisasi, akijiweka karibu na Urusi na Uchina.

A handout photo made available by Iraq's military-run Security Media Cell via Facebook shows the remains of a burning vehicle beside a tall concrete wall. The hulk of wheels and the bonnet can be made out, with the main bulk of the vehicle in flames. The tall wall with railings on the top is behind the vehicle. It is night and orange flames illuminate the area.

Chanzo cha picha, Iraq Security Media Cell via EPA

Mnamo mwaka wa 2025, Israel ilichukua hatua za kijeshi dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran, na kuwauwa wanasayansi, wanajeshi na maafisa wa ngazi za juu, ikiwa ni pamoja na kutekeleza mashambulizi yanayoongezeka katika maeneo ya makazi.

Iran ililipiza kisasi kwa kurusha makombora dhidi ya Israel.

A handout satellite image made available by Maxar Technologies shows a close-up view of holes and craters on a ridge at the Fordo underground uranium enrichment site following US airstrikes. Three circular craters are in a straight line at the top of the image and three forming a triangle are at the bottom. The surrounding ground is grey and brown.

Chanzo cha picha, Maxar via EPA

Marekani ilipojiunga na mashambulizi ya Israel, Khamenei aliapa kutojisalimisha, lakini alionekana dhaifu.

Tarehe 28 Februari 2026, Marekani na Israel kwa pamoja zilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya Iran. Trump alihalalisha mashambulizi hayo, akisema Iran “kamwe haiwezi kuwa na silaha ya nyuklia”.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alisema hatua hiyo ni kuondoa ’tishio lililopo’ linalosababishwa na Iran.

Israel ilisema Iran ilianzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi huko, huku milipuko ikitokea katika mataifa kadhaa ya Ghuba.

Woman dressed in black robes gather in an outdoor public area on 14 January 2026. Three of them are holding posters of Khamenei.

Chanzo cha picha, Abedin Tahaerkenareh / EPA

Khamenei ametawala siasa za Iran, akionyesha udhibiti na mara nyingi kulitokea ukatili kwa waliokuwa madarakani.

Wakati fulani, Kiongozi Mkuu alijidhihirisha kuwa karibu juu ya siasa – akidharau ugomvi kati ya wanamageuzi na wahafidhina.

Lakini mara chache Ayatollah Khamenei aliruhusu upinzani kwa sera ambazo alikataa kuendeleza.

Maisha ya Iran yanatawaliwa na sheria alizoziweka. Ni wachache sana wanaoweza kusema ni mabadiliko gani yatarajiwe.

Imetafsiriwa na Asha Juma na kuhaririwa na Ambia Hirsi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *