Mkuu wa Majeshi wa Iran, Waziri wa Ulinzi, na Kamanda wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi wameuawa katika mashambulizi ya Marekani na Israeli.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa majeshi ya Iran, Abdolrahim Mousavi, aliuawa pamoja na majenerali wengine wa ngazi za juu katika mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel dhidi ya nchi hiyo, televisheni ya serikali imeripoti leo Jumapili Machi Mosi.

Televisheni ya serikali imetaja jina la Abdolrahim Mousavi miongoni mwa maafisa wakuu waliouawa siku ya Jumamosi, pamoja na Waziri wa Ulinzi na mkuu wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi, Mohammad Pakpour, na Ali Shamkhani, mshauri wa Kiongozi Mkuu, ambaye vifo vyao vilikuwa vimethibitishwa hapo awali.

Televisheni ya serikali imesema kwamba waliuawa “wakati wa mkutano wa Baraza la Ulinzi,” na kuongeza kwamba majina mengine yatatangazwa baadaye.

Wakati Marekani na Israel zikizindua wimbi la mashambulizi dhidi ya Iran Jumamosi, Februari 28, vyombo vya habari vya serikali ya Iran vilitangaza Jumapili, Machi 1, kifo cha Ayatollah Ali Khamenei, kikithibitisha taarifa iliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na Rais wa Marekani Donald Trump

Wakati huo huo Tehran inaendelea kushambulia kambi za kijeshi za Marekani katika eneo hilo na nchini Israel, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti. Vifo vya mkuu wa jeshi la Iran Abdolrahim Mousavi, waziri wa ulinzi Mohammad Pakpour, kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na Kiongozi Mkuu Ali Shamkhani pia vimethibitishwa.

Afisa mkuu wa usalama wa Iran aonya dhidi ya majaribio ya kuigawanya nchi

Afisa mkuu wa usalama wa Iran, Ali Larijani, ameonya leo Jumapili dhidi ya majaribio ya kuigawanya nchi kufuatia kifo cha Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei, aliyeuawa katika mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel: “Makundi yanayotaka kuigawanya Iran yanapaswa kujua kwamba hatutavumilia,” almeema Larijani, mkuu wa Baraza Kuu la Usalama wa Kitaifa, katika mahojiano yaliyorushwa kwenye televisheni ya serikali, akiwataka Wairan kuungana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *