Kiongozi wa juu wa kiroho wa Iran ameuawa katika shambulio la Israeli na Marekani- Televisheni ya inayomilikiwa na serikali ya Iran.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Iran imetangaza siku 40 za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha kiongozi wake wa juu wa kiroho Ayatollah Ali Khamenei.

Aidha imetangaza siku nyengine saba za mapumziko ya kitaifa kuomboleza kifo cha Ayatollah ambaye amekuwa madarakani tangu mwakwa wa 1989.

Vyombo vya habari vya Iran pia vimeripotiwa kwamba binti wa Khamenei , mkwe wake na mjukuu wake wameuawa katika mashambulizi ya Marekani na Israel.

Iran imeapa kutoa adhabu kali kwa wale imewataja kama wauaji wa Khamenei.

Naye Rais wa Marekani Donald Trump ambaye nchi yake na Israel zilihusika katika shambulio nchini Iran amesherekea kuuawa kwa kiongozi wa Iran.

Licha ya kuthibitisha kuuawa kwa Khamanei, Trump amesisitiza kwamba wataendelea kutekeleza mashambulio nchini Iran.

Nao Raia wa Iran wamekusanyika  katika Uwanja wa Enghelab, kuomboleza kifo cha kiongozi wao wa  Kiroho Ayatollah Ali Khamenei aliyeuawa katika mashambulio ya Israel na Marekani Jumamosi, mjini Tehran, Iran, Machi 1, 2026.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *