Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Ali Larijani amesema taifa hili litazifanya Marekani na Israel kujutia uchokozi wao dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Larijani amesema hayo kwenye ujumbe alioutuma kwenye akaunti yake ya mtandao wa X jana Jumamosi na kueleza kuwa, “Tutawafanya wahalifu wa Kizayuni na Wamarekani wanaodharauliwa wajutie matendo yao.”

Dakta Larijani ameeleza bayana kuwa: Wanajeshi mashujaa na taifa kubwa la Iran watatoa somo lisilosahaulika kwa mashetani na madikteta wa kimataifa.

Mapema jana, Marekani na Israel zilifanya mashambulizi ya anga katika miji mbalimbali katika majimbo 24 ya Iran, yakilenga maeneo ya kijeshi na maeneo ya makazi, miongoni mwa maeneo mengine.

Kwa mujibu wa tangazo la Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran, zaidi ya watu 200 wamethibitishwa kuuawa shahidi kufikia saa mbili usiku wa kuamkia leo. Idadi ya waliojeruhiwa ni zaidi ya 800.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *