Kundi la makamanda wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kulingana na taarifa ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, jana kundi la makamanda jasiri na mashujaa wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameuawa shahidi katika shambulio la kikatili la Marekani mhalifu na utawala wa Kizayuni.

Ifuatayo ni Taarifa Kamili ya Taasisi ya Kuhifadhi Kumbukumbu na Kueleza Maadili ya Vita Vitakatifu na Muqawama

“Kwa Jina la Mola wa Mashahidi na Wenye Ukweli

Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo. (Sura Al-Ahzab – Aya ya 23)

Taifa Tukufu na Adhimu la Iran,

Kwanza tunatoa pole kwa msiba wa kufa shahidi kiongozi jasiri, mwenye busara, na mpiganaji asiyekata tamaa wa Iran na ulimwengu wa Kiislamu, Ayatullah Al-Uzma Imam Khamenei (Mwenyezi Mungu amrehemu). Jana, kundi la makamanda jasiri na mashujaa wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliuawa shahidi katika shambulio la kikatili la madhalimu wabaya zaidi, wauaji, na wafisadi duniani, Marekani mhalifu na utawala wa Kizayuni.

Miongoni mwa waliouawa shahidi ni

  • Meja Jenerali Shahidi Seyed Abdulrahim Mousavi, Mkuu wa Kamandi ya Majeshi
  • Meja Jenerali Shahidi Mohammad Pakpour, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
  • Admeri Ali Shamkhani, Mshauri wa Amiri Jeshi Mkuu na Katibu wa Baraza la Ulinzi.
  • Amiri Sar-Lashkar Shahidi Aziz Nasirzadeh, Waziri wa Ulinzi na Usaidizi wa Vikosi vya Silaha.

Hao walikuwa miongoni mwa mashahidi walioitikia mwito wa Mwenyezi Mungu wakati wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Ulinzi, na wamejiunga na wenzao waliotangulia waliouawa shahidi.

Bila shaka, taifa tukufu na kuu la Iran, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kwa neema ya Bwana wetu wa Zama (Nyoyo zetu ziiwe muhanga kwa ajili yake), wataendelea kuwa imara katika njia yenye nuru ya Imam Khomeini (Ruhullah) na Imam wa Mashahidi, Ayatullahil Udhma Imam Khamenei (Mwenyezi Mungu amrehemu). Watafanikiwa kuzima njama zote za maadui walioapa, na wataiongoza Iran ya Kiislamu kupitia kipindi hiki muhimu cha kihistoria kwa ushindi na mamlaka makubwa.

Majina ya mashahidi wengine wapendwa yatatangazwa baadaye.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *