.

Chanzo cha picha, Airbus DS 2026

    • Author, Hafsa Khalil
  • Muda wa kusoma: Dakika 6

Rais Donald Trump amesema Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amefariki saa chache baada ya Marekani na Israel kufanya mashambulizi makubwa nchini humo.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hapo awali alisema makao ya Khamenei Tehran yameharibiwa katika “shambulio kali na la kushtukiza” na kwamba kuna dalili kwamba kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 86 “hayupo tena”.

Kifo cha Khamenei kilitangazwa baadaye kwenye televisheni ya taifa ya Iran.

Iran ilijibu mashambulizi kwa kurusha makombora na ndege zisizo na rubani kuelekea Israel na nchi nne za Kiarabu ambazo zina kambi za kijeshi za Marekani: Bahrain, Kuwait, Qatar na UAE.

haya ndio tunayojua kufikia sasa

Ni nini kinafanyika Iran?

People head for cover in Tehran.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Muda mfupi baada ya saa tatu unusu asubuhi (saa za Tehran) sawa na (06:00 GMT), Shirika la Habari la Iran liliripoti milipuko katika mji Mkuu wa Tehran.

Picha zilizoonekana na BBC zinaonyesha moshi ukifuka kwenye uwanja wa Jomhouri mjini na Hassan Abad Square.

Milipuko pia iliripotiwa kusikika katika miji mingine kadhaa kote nchini, ikijumuisha: Isfahan, Qom, Karaj, na Kermanshah. Kiwango cha majeruhi au uharibifu wowote hakijabainika kufikia sasa.

Aanga ya Iran imefungwa tangu mashambulizi Yyalipoanza, Shitika la Habari la Tasnim lilisema.

Trump ameelezea operesheni hiyo kuwa “kubwa na inayoendelea”.

Video kadhaa zilizothibitishwa na BBC Verify zinaonyesha moshi mkubwa ukifuka kote Tehran.

BBC Verify imeweza kufuatilia na kuthibitisha video moja ikionyesha kombora lililivyopiga eneo karibu na Jumba la Ledership, ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei. Video hiyo hata hivyo hainyeshi moja kwa moja ikiwa kombora hilo lililenga jengo hilo moja kwa moja.

Picha nyingine iliyothibitishwa kutoka eneo hilo hilo inaonyesha moshi mweusi ukifuka juu ya majengo ya makazi na maduka madogo yanayouza bidhaa za vyakula. Pia kuna ripoti za mashambulio hayo kushuhudiwa katika maeneo mengine ya Iran.

A map of the cities that have reportedly been struck.

Marekani na Israel zimesema nini ?

Trump aliweka video kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kuthibitisha kuhusika kwa Marekani katika shambulio hilo.

“Muda mfupi uliopita, jeshi la Marekani limeanzisha operesheni kubwa ndani ya Iran ,”alisema.

”Ninasema usiku wa leo kwamba uhuru wenu umekaribia. Endelea kujikinga. Usiondoke nyumbani kwako. Ni hatari sana nje. Mabomu yatarushwa kila mahali.” alisema Rais Trum katika taarifa baada ya kuthibitisha kuanzishwa kwa operesheni kubwa ya kijeshi nchini Iran.

”Tukimaliza, kuangusha serikali yenu. Itakuwa nafasi yenu kuchukua. Labda hii itakuwa nafasi yako pekee kwa vizazi. Kwa miaka mingi mmeomba usaidizi wa Marekani lakini humkuupata. Hakuna rais aliyekuwa tayari kufanya kile ambacho niko tayari kufanya usiku wa leo. Sasa una rais ambaye anakupa unachotaka. Basi hebu tuone jinsi mnavyojibu.” aliendelea kusema Trump.

”Markani inawaunga mkono kwa nguvu nyingi na. Sasa ni wakati wa kuchukua udhibiti wa hatima yanu na kuachilia mustakabali wenye mafanikio na utukufu ambao uko karibu na wewe kufikia.” alisema.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pia alitoa wito kwa Wairan wote “kupiga moyo konde na kujiokoa dhidi ya dhulma wanazofanyiwa na kukumbatia Iran huru na yenye amani”.

Akimshukuru Trump, alikariri ujumbe wake kwamba Iran “haitaruhusiwa kuwa na silaha za nyuklia ambazo zitaiwezesha kutishia ulimwengu mzima”.

“Hatua yetu ya pamoja itaunda mazingira kwa watu jasiri wa Iran kuchukua hatima yao mikononi mwao.”

Pia aliwashauri raia wa Israel kufuata miongozo kutoka kwa mamlaka.

Hapo awali, waziri wa ulinzi wa Israel alitangaza “hali ya dharura ” kote Israel.

Iran imejibu vipi?

Jeshi la Israel linasema kuwa limetambua makombora yaliyorushwa na Iran kuelekea Israel, likisema linafanya kila iwezalo “kuzuia na kushambulia vitisho ikilazimika kufanya hivyo”.

Milipuko imesikika katika mji wa Haifa na kwingineko nchini Israel, lakini haijabainika kwa sasa ikiwa haya yalikuwa athari au uvamizi.

Huku hayo yakijiri katika eneo hilo, shirika la habari la serikali la Bahrain liliripoti kushambuliwa kwa kambi ya Jeshi la Wanamaji laMarekani, ambalo liko Bahrain, “limeshambuliwa kwa kombora”.

Haya yanajiri baada ya wizara ya mambo ya ndani ya Bahrain kusema ving’ora vya dharura vimepigwa, na kuwataka wakaazi kuwa watulivu na kuelekea sehemu salama iliyo karibu zaidi.

Wizara ya ulinzi ya Qatar ilisema “ilifanikiwa kukabiliana na mashambulizi kadhaa yaliyolenga eneo la nchi hiyo”, vyombo vya habari vya serikali viliripoti, baada ya milipuko kusikika katika mji mkuu wa Doha.

Qatar ni mwenyeji wa kambi ya kijeshi ya Al Udeid, kituo kikubwa zaidi cha kijeshi cha Marekani katika eneo hilo la mashariki ya kati.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imelaani katika taarifa yake “ukiukaji wa wazi” wa anga yake uliofanywa na Iran katika shambulio la kombora.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Qatar “inahaki ya kujibu.”

Waisraeli wameonywa dhidi ya mikusanyiko na kuenda shule au kazini kama sio muhimu. Mwongozo huo uitadumishwa hadi Jumatatu 20:00, mamlaka imesema.

Anga ya Israel pia imefungwa kwa ndege za kiraia, kulingana na vyombo vya habari vya Israeli.

Map of Middle East.

Ni salama kusafiri katika eneo hilo?

Baadhi ya mashirika ya ndege ya kimataifa yamesitisha safari kuelekea maeneo tofauti Mashariki ya Kati.

Shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa lilisema limesitisha safari za ndege za kwenda-na-kutoka Dubai mwishoni mwa juma, pamoja na miji mikuu ya Israel, Lebanon na Oman hadi tarehe 7 Machi.

Wizz Air vile vile imesitisha safari zake hadi Machi 7 katika Israeli, Dubai na Abu Dhabi na Amman huko Jordan.

Virgin Atlantic imesema kuwa haitatumia anga ya Iraq kwa muda, na imeahirisha safari ya ndege siku ya Jumamosi kutoka London Heathrow hadi Dubai.

Mamlaka ya usafiri wa anga ya Kuwait imetangaza kusitisha safari zote za ndege kwenda Iran hadi ilani nyingine itakapotolewa, kulingana na vyombo vya habari vya serikali.

Baadhi ya nchi katika eneo hilo – ikiwa ni pamoja na Iraq na Jordan – pia zimefunga anga zao.Falme za Kiarabu, UAE ilisema “imefunga kwa muda” anga yake kama hatua ya tahadhari, vyombo vya habari vya serikali viliripoti.

Wakati huo huo, mwongozo wa usafiri wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza kwa Jordan, Syria, Lebanon, Iraq, Yemen, Uturuki, Saudi Arabia na Oman, sasa inawashauri wasafiri “kukaa macho, kufuata ushauri wa mamlaka ya ndani na kupata makazi ikiwa watashauriwa”.

Ulimwengu ulivyopokea shambulio

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas ametaja matukio ya hivi punde kuwa “hatari”.

“EU imepitisha vikwazo vikali dhidi ya Iran na kuunga mkono suluhu za kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na suala la nyuklia,” alisema katika taarifa yake kwenye mtandao wa X, na kuongeza kuwa amezungumza na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Israel na wengine wa kikanda.

“Tunaipatia ulinzi wa raia na sheria ya kimataifa ya kibinadamu kipaumbele.”

Msemaji wa serikali ya Uingereza alisema wanapinga “kuongezeka zaidi kwa mzozo wa kikanda”.

“Kipaumbele yetu kuu ni usalama wa raia wa Uingereza katika kanda hiyo,” taarifa hiyo ilisema, lakini ikaongeza: “Tuko tayari kulinda masilahi yetu.”

Waziri Mkuu Keir Starmer ameongoza kikao cha kamati ya dharura ya serikali, na anatarajiwa kuwasiliana na washirika waUingereza kwa njia ya simu siku nzima.

BBC inafahamu kuwa Uingereza haikuhusika katika mashambulizi ya Marekani na Israel.

Ujerumani imesema kuwa iliarifiwa kuhusu shambulio hilo mapema asubuhi ya leo ,na kwamba Kansela Friedrich Merz ameshauriana na Mawaziri husika wa usalama.

Kufuatia wito wa mkutano na mawaziri na wakuu wa kijasusi, ofisi ya Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni ilisema itashauriana na washirika na viongozi wa kikanda ili kuunga mkono juhudi za kupunguza mvutano.

Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese alisema nchi yake inaunga mkono hatua ya Marekani “kuzuia Iran kupata silaha za nyuklia na kuzuia Iran kuendelea kutishia amani na usalama wa kimataifa”.

Wakati huo huo, Urusi imelaani mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, na kuyataja kuwa ni “hatua ya kiholela”.

“Piaililaani vikali hatua hiyo ikisema mashambulizi hayo kwa mara nyingine tena yanafanywa chini ya kivuli cha mchakato mpya wa mazungumzo,” wizara ya mambo ya nje ilisema, ikiashiria mazungumzo ya nyuklia ya Marekani na Iran ambayo yalifanyika siku ya Ijumaa.

Taarifa hiyo pia imeitaka jumuiya ya kimataifa kufumbia macho kile ilichokiita kuwa “vitendo vya kutowajibika vinavyolenga kudhoofisha amani, utulivu na usalama” katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *