- Mbunge Johanna Ngeno alifariki kwenye ajali ya helikopta katika msitu wa Chepkiep, Mosop, alipokuwa akitathmini uharibifu wa mafuriko kando ya Mto Mara
- Video iliyoibuliwa upya ilimuonyesha akizungumza kuhusu maisha ya baada ya kifo, akisema kulikuwa na mahali pazuri zaidi ya maisha haya
- Matamshi yake yalizua hisia tofauti mtandaoni, baadhi ya wakiyataja kuwa ya kinabii ya kutisha huku wengine wakiyaona kama mafumbo ya kisiasa
Mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ngeno alipoteza maisha yake kwa msiba Jumamosi, Februari 28, kufuatia ajali ya helikopta, na kutumbukiza taifa zima katika maombolezo.

Source: Facebook
Ajali hiyo ilitokea alipokuwa akikagua uharibifu uliosababishwa na mafuriko katika maeneo ya kando ya Mto Mara.
Watu sita walipoteza maisha, akiwemo mpiga picha wake, mwalimu mmoja na rubani.
Video iliyorekodiwa ndani ya helikopta kabla ya ajali ilisambaa mtandaoni, ikionyesha waliokuwamo wakiwa na furaha na hali ya juu kabla ya mkasa huo kutokea.
Johanna Ngeno alisema nini kuhusu maisha ya baada ya kifo?
Baada ya kifo chake, Wakenya walianza kurejelea hotuba zake za awali. Hotuba moja hasa ilivutia hisia za wengi, huku baadhi wakijadili kama maneno yake yalikuwa na maana ya kina zaidi.
Katika video iliyosambaa tena, iliyorekodiwa alipokuwa akihutubia wakazi wa Ololmasani Ijumaa, Februari 27, Ngeno alizungumzia kwa kina kuhusu maisha baada ya kifo.
Akiwa kama mhubiri, alitafakari kuhusu maisha ya milele, akieleza kuwa hata kama maisha ya hapa duniani yanaonekana mazuri, kuna mahali bora zaidi mbinguni.
Akitumia mfano wa Yesu katika Biblia, alieleza kwamba kusema ukweli mara nyingi huja kwa gharama.
Kwa maneno yaliyotafsiriwa:
“Kuna mahali bora zaidi kuliko hapa tunapoishi. Hata Yesu aliishi duniani kwa miaka 33, na alizungumza ukweli uliompelekea kuuawa. Lakini alisema kifo si mwisho, kwa sababu alikuwa anarudi nyumbani.”
Aliendelea kusisitiza kuwa mbinguni ni mahali halisi, akisema Yesu asingewaahidi watu wake kuhusu mahali hapo kama halingekuwepo.
“Yesu aliahidi kwamba angerudi siku moja kuwachukua watu wake waende pamoja naye. Alisema kama mahali hapo pasingekuwepo, asingewaambia. Vivyo hivyo, ninawaambia kwamba ingawa hapa ni pazuri na patamu, kuna mahali patamu zaidi kuliko hapa. Nimefika huko na nimeona mwenyewe. Nitakaporudi, nitawachukua mwende huko ili pale nilipo, nanyi muwepo. Kama mahali hapo pasingekuwepo, nisingewaambia. Siwezi kuwahadaa. Lakini nawathibitishia, kuna mahali patamu zaidi.”

Pia soma
Johanna Ng’eno: Shahidi asema helikopta iliyomuua mbunge ililipuka mara baada ya kutua kwa dharura
Wakenya watoa maoni
Kauli zake zimezua maoni mseto mtandaoni.
Baadhi ya Wakenya walieleza kuwa hotuba hiyo inashtua sana hasa ikizingatiwa kifo chake cha ghafla, wakihisi kana kwamba ilikuwa kama unabii.
Wengine walidai huenda alikuwa akizungumza kwa mafumbo ya kisiasa, akirejelea azma ya kuwania wadhifa wa juu zaidi baada ya kuhudumu mihula mitatu kama Mbunge.
GK Kechwo alisema: “Ilikuwa hotuba ya mfano kuhusu kuwania kiti cha juu zaidi, lakini sasa imechukua maana nyingine.”
Kiplangat Benson aliandika: “Labda aliona kinachokuja.”
Charlotte Tapkigen alisema: “Nilihisi alikuwa akizungumzia kuingia katika ofisi kubwa siku zijazo. Alikuwa na mipango ya kuwania cheo kikubwa.”
Neddy Chepkorir aliuliza: “Alikuwa anahisi kifo chake kinawadia? Alikuwa ametishiwa?”
Chemutai Melody alisema: “Maisha ni ya kiroho sana. Pole Ngong.”
Hillary Kipyator Kipkorir aliandika: “Waaah, kama vile alitabiri!”

Source: Facebook
Ujumbe wa mwisho wa Johanna Ngeno kwa rafiki yake
Katika taarifa iliyochapishwa na TUKO.co.ke, rafiki yake wa karibu, GK Kechwo, alishiriki ujumbe wa mwisho alioupokea kutoka kwa mwanasiasa huyo.

Pia soma
Chapisho la mwisho la Johanna Ngeno mitandaoni laibuka baada ya kufariki katika mkasa wa helikopta
Kulingana na Kechwo, Ngeno alimtumumia eneo (location) walilopaswa kukutana kabla ya kusafiri pamoja katika helikopta hiyo iliyopata ajali.
Hata hivyo, Kechwo alichelewa njiani na akakosa safari hiyo kwa takribani dakika tano.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke
