SHINYANGA: WANANCHI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wameaswa kuwapa nafasi vijana na watoto kushiriki michezo kwani kufanya hivyo itawasaidia kupata mwanga na kufikia ndoto katika vipaji vyao.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Peter Masindi alisema kwenye tamasha la amani na maendeleo ambalo limefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Buduhe nakuratibiwa na halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

Masindi amesema Shirikisho la soka la Mpira Tanzania (TFF ) ipo Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuinua na kukuza vipaji vya watoto kupitia uanzishwaji wa Shule za michezo mbalimbali.

“Leo hii tunapozungumza TFF ipo Mkoa wa Shinyanga na wanafanya mkutano wao mkubwa Kahama lengo lao likiwa ni kuanzisha Shule za akademi hivyo nawaomba wananchi muwaache watoto wafanye michezo,” amesema Masindi.

Masindi amesema watoto wakijifunza na kuelewa michezo hiyo itakuwa ni mwanga utakaowasaidi kupata ajira na kujikwamia kiuchumi.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Lucy MAyenga amesema kupitia bonanza hilo ameshudia vipaji mbalimbali ikiwemo mchezo wa mpira wa Miguu ,kukimbiza kuku,kucheza drafti hali inayoleta motisha kwa viongozi kuongeza nguvu katika kuboresha vipaji hivyo.

Mayenga amewakumbusha Viongozi na wadau mbalimbali kuinua vipaji na kuwashika mkono kadrii iwezekanavyo ili kuhakilisha watoto wanafika pale wanatamani kuwepo.

“Nawaomba viongozi na wadau mbalimbali tujitokeze kuwashika mkono watoto katika michezo tukishirikiana kwa pamoja tutaweza kulifanikisha hili” amesema Mayenga.

Nao baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia michuano hiyo akiwemo John Mange mkazi wa Kitongoji Cha Mwasele Mhunze Wilaya ya Kishapu amesema wamefurahishwa na vipaji mbalimbali ambavyo vimeoneshwa katika bonanza hilo la michezo na kwamba wanatamani kuwaona wanafika mbali hasa kisoka.

Mbonanza la michezo mbalimbali limefanyika katika Halmashauri ya Kishapu kwa kuwahisisha watoto mpaka wazee ,kwa kunzingatia jinsi pamoja na makundi maalumu kwa lengo la kuhamasisha amani na maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *