WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, amekagua ujenzi wa barabara ya Mbulu – Garbabi (km 25), ambayo ni sehemu ya mradi wa barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 389) unaojengwa kwa kiwango cha lami.

Mradi huo unatekelezwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa lengo la kuboresha mawasiliano ya barabara, kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi katika maeneo husika. SOMA: Tanroads Manyara yajizatiti ukarabati barabara

Taarifa ya mradi inaonyesha kuwa hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 41.7. Jumla ya shilingi bilioni 36.3 zinatarajiwa kutumika kukamilisha ujenzi huo, huku malipo ya shilingi bilioni 12.5 yakiwa tayari yameshafanyika. Ukamilishaji wa barabara hiyo unatarajiwa kuongeza ufanisi wa usafiri na kuimarisha shughuli za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa maeneo yanayounganishwa na barabara hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *