.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Shambulio lililomuua kiongozi mkuu wa Iran halikutokea usiku wa manane, kama ilivyotarajiwa, lakini katikati ya asubuhi.

Hii ni kwa sababu Marekani na Israel ziliamua kuchukua fursa ya sehemu muhimu ya kijasusi iliyofika saa chache kabla ya tukio hilo.

Kwa miezi kadhaa walisubiri fursa wakati maafisa wakuu wa Iran wangekusanywa pamoja na kujua kwamba Kiongozi Mkuu Ali Khamenei angekuwa kwenye boma moja katikati mwa mji wa Tehran Jumamosi asubuhi.

Pia walijua eneo la maafisa wengine wa ngazi za juu wa kijeshi na ujasusi ambao wangekutana kwa wakati mmoja.

Kwa miezi kadhaa, nchi zote mbili zilifuatilia mienendo ya kiongozi huyo mkuu, ambaye alitawala Iran tangu 1989. Mbinu kamili walizotumia ni siri, ingawa Rais Donald Trump aligusia kitu katika chapisho la mtandao wa kijamii.

“Hakuweza kukwepa ujasusi na mifumo yetu ya ufuatiliaji wa hali ya juu,” alitoa maoni.

Inaweza kuwa chanzo ni mwadamu , lakini kuna uwezekano zaidi kwamba ilikuwa ufuatiliaji wa kiufundi wa watu binafsi.

Katika vita vya siku 12 mwezi Juni uliopita, Israel ililenga wanasayansi na maafisa wanaohusishwa na mpango wa nyuklia wa Iran na inasemekana ilitumia upenyezaji wa mifumo ya mawasiliano ya simu na simu za mkononi kuelewa mienendo ya watu.

Wakati mwingine hatua hiyo ilihusisha kufuatilia mienendo ya walinzi wanaohusishwa na maafisa wa ngazi za juu.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa muda mrefu, hii inaweza kusaidia kujenga “mtindo wa maisha” kutabiri na kuelewa shughuli, na pia kutambua nyakati za hatari.

Iran ilijua kwamba kiongozi huyo mkuu yuko machoni mwa maadui zake, na kwa hivyo kushindwa kutambua na kushughulikia udhaifu huu katika miezi ya hivi karibuni kunaonyesha aidha kushindwa kwa kiasi kikubwa katika usalama wa Iran na kukabiliana na ujasusi, au uwezo wa Israel na Marekani kuendelea kurekebisha mbinu zao na kutafuta njia mpya za kufuatilia.

Huenda Wairani pia walifikiri kuwa shambulio la mchana lilikuwa na uwezekano mdogo. Katika kesi hiyo, taarifa za kijasusi, kwa mujibu wa gazeti la The New York Times, zilitoka kwa CIA lakini zikapewa Israel kutekeleza shambulio hilo.

Shambulio dhidi ya Ayatollah Khamenei

Kila kitu kinaonyesha kuwa kuna mgawanyiko wa majukumu: Israeli inazingatia mashambulizi dhidi ya viongozi na Marekani inalenga maeneo ya ijeshi .

Intelejensia ilitoa taarifa za kutosha kutabiri mienendo ya kiongozi mkuu na maafisa wengine kwa kupanga shambulio na ndege yenye uwezo wa kurusha makombora ya masafa marefu.

Badala ya shambulio moja dhidi ya Ayatollah Khamenei, mpango ulikuwa wa shambulio la kwanza la bomu ili kuanzisha kampeni pana zaidi ya kijeshi, na ilitumiwa ili kutumia fursa iliojitokeza.

Ndege za Israel huchukua takriban saa mbili kufika Tehran, lakini haijabainika zilitumia umbali gani kutekeleza shambulizi.

Iliripotiwa kuwa ndege za Israel zilitumia mabomu 30 kushambulia boma alikokuwa kiongozi mkuu mwendo wa saa 9:40 asubuhi kwa saa za huko.

Hii ni kwa sababu kiongozi mkuu alitumia chumba cha chini ya ardhi kwa ajili ya ulinzi (ingawa chumba hicho hakikuwa moja ya vyumba vya chini zaidi ya ardhi katika utawala).

Mashambulizi mengi ya risasi yanaweza kuwa yalipenya kwa kina cha kutosha ili kuhakikisha kuwa shabaha iliafikiwa.

Maeneo mengine katika mji mkuu wa Iran pia yalishambuliwa, ikiwa ni pamoja na ofisi ya Rais Masoud Pezeshkian, ambaye baadaye alitoa taarifa akisema yuko salama.

Israel imesema maafisa saba wakuu wa ulinzi wa Iran ni miongoni mwa waliofariki akiwemo Katibu wa Baraza la Ulinzi Ali Shamkhani, Waziri wa Ulinzi Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh na kamanda wa IRGC Jenerali Mohammad Pakpour.

Wakati ndege hizo ziliposhambulia, ilikuwa usiku wa manane huko Mar-a-Lago, Florida, ambapo Trump alikuwa amekutana na baadhi ya maafisa wake wakuu kufuatilia maendeleo.

Baada ya saa kadhaa ilithibitishwa kwamba kiongozi mkuu alikufa katika mashambulizi hayo.

Iran ilikuwa tayari imejiandaa kwa uwezekano huu, huku ripoti zikionyesha kwamba mipango ya urithi ilikuwa tayari imewekwa sio tu kwa kiongozi mkuu, bali pia kwa maafisa kadhaa wakuu.

Hiyo ina maana bado haijulikani kifo hiki kitamaanisha nini katika kipindi cha mzozo huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *