
Jeshi la Israel limeonya leo Jumatatu kwamba linapanga “kuongeza” mashambulizi yake nchini Lebanon likilenga Hezbollah kama kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya roketi ya vuguvugu hili la Washia kuelekea eneo lake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Mashambulizi yanaendelea na yataimarishwa,” ameandika Jenerali Rafi Milo, mkuu wa Kamandi ya Kaskazini, katika taarifa ya jeshi kwenye Telegram, akibainisha kwamba vuguvugu hilo la Washia “litalipa gharama kubwa” kwa msaada wake kwa Tehran.
Kundi la Hezbollah, kwa upande wake, limethibitisha kurusha makombora na ndege zisizo na rubani kutoka Lebanon kuelekea Israel.
Hezbollah linasema hatua hiyo ni ya kulipiza kisasi mauaji ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei.
Makombora hayo yalianguka katika maeneo ya wazi katika eneo la Israel, kulingana na Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF).
Katika taarifa, Jeshi hilo limeishutumu Hezbollah kwa kufanya kazi kwa niaba ya Iran na kuwalenga raia wa Israel.
IDF imeongeza kuwa vitendo vya Hezbollah vinaweza kusababisha uharibifu nchini Lebanon na kusema kwamba itajibu kwa nguvu zote mashambulio yanayoendelea.