Mashambulizi ya Israeli na Marekani yamewaua watu wasiopungua 555 nchini Iran tangu yalipoanza Jumamosi, Februari 28, Shirika la Hilali Nyekundu la Iran limetangaza leo Jumatatu, Machi 2. Mgogoro huo sasa umeenea hadi Lebanon, ambapo jeshi la Israel limeshambulia ngome za Hezbollah kwa mabomu kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora yaliyotekelezwa na kundi hili la Washia katika eneo lake. 

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Washington na Tel Aviv zinaendelea na mashambulizi na operesheni zao dhidi ya Iran, huku Israel ikidai kuwa tayari “imewaangamiza maafisa 40 wa ngazi za juu” wa Iran, akiwemo Kiongozi Mkuu Ali Khamenei, katika operesheni hiyo.

Angalau watu 555 wameuawa kote Iran tangu kuanza kwa mashambulizi ya Marekani na Israel siku ya Jumamosi, shirika la Hilali Nyekundu la Iran limetangaza leo Jumatatu, Machi 2. Kwa jumla, “miji 131 imeathiriwa hadi sasa,” shirika hili la kibinadamu limeongeza katika ujumbe uliotumwa kwenye Telegram.

Tangu Jumamosi, Februari 28, Israel na Marekani zimekuwa zikifanya mashambulizi ya anga dhidi ya mji mkuu wa Iran, Tehran. Kiongozi Mkuu Ali Khamenei aliuawa katika shambulio la Israel na Marekani siku ya Jumamosi. Kufuatia tangazo hili, Jamhuri ya Kiislamu ilitangaza siku 40 za maombolezo na siku saba za mapumziko. Televisheni ya serikali ya Iran pia iliripoti siku ya Jumapili vifo vya maafisa wengine wanne.

Maafisa watatu wakuu wa Iran watasimamia mpito nchini Iran kufuatia kifo cha Kiongozi Mkuu Ali Khamenei, mmoja wa washauri wake alitangaza, kama alivyonukuliwa na televisheni ya serikali. Watatu hawa ni Rais Massoud Pezeshkian, mkuu wa mahakama, Gholamhossein Mohseni Ejei, na mtaalamu wa sheria kutoka Baraza la Walinzi.

Wanajeshi watatu wa Marekani waliuawa na wengine watano kujeruhiwa vibaya, kamanda mkuu wa Marekani (Centcom) ametangaza, majeruhi wa kwanza wa Marekani wanaojulikana katika mzozo huo. Jeshi la Israel pia limetangaza kuwa litahamasisha wanajeshi 100,000 wa akiba na “kuimarisha utayari wake katika pande mbalilba za mapigano.”

Wakuu wa nchi za Ufaransa, Ujerumani, na Uingereza, katika taarifa ya pamoja iliyotolewa siku ya Jumapili, walitangaza kwamba wako tayari kwa “vitendo vya kujilinda vinavyolingana” ili “kuharibu uwezo wa Iran wa kurusha makombora na ndege zisizo na rubani kutoka chanzo chake.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *