Milipuko kadhaa imesikika leo Jumatatu karibu saa 11:00 Alfajiri  huko Jerusalemu, ambapo ving’ora vimesikika baada ya jeshi kutangaza urushaji wa makombora ya Iran kuelekea Israel, waandishi wa habari wa AFP wameripoti.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Milipuko pia imesikika katika eneo la Tel Aviv, katikati mwa Israel.

“Muda mfupi uliopita, vikosi vya jeshi la Israel vilitambua makombora yaliyorushwa kutoka Iran kuelekea Israel,” jeshi limesema, na kuongeza kuwa ulinzi wa anga ulikuwa umewashwa ili kuyazuia, na kuwasihi raia kujificha.

Bahrain yatangaza kifo cha mtu mmoja aliyeuawa katika mashambulizi ya Iran

Bahrain imetangaza leo Jumatatu kwamba mtu mmoja ameuawa katika mashambulizi ya Iran, kifo cha kwanza nchini, na kusababisha idadi ya vifo katika majimbo ya Ghuba kufikia watano tangu siku ya Jumamosi.

“Moto ulizuka ndani ya meli ya kigeni katika jiji la viwanda la Salman baada ya vifusi vya kombora lililozuiliwa kuanguka ndani ya meli. Moto huo ulisababisha kifo cha mfanyakazi mmoja wa Asia na majeraha makubwa kwa wengine wawili,” Wizara ya Mambo ya Ndani imesema, na kuongeza kuwa moto huo “umedhibitiwa na kuzimwa.”

Milipuko yasikika Doha, Dubai, na Bahrain

Milipuko mikubwa imesikika leo Jumatatu katika miji ya Ghuba ya Uajemi ya Dubai, Doha, na Manama, huku Tehran ikianza siku ya tatu ya mashambulizi dhidi ya majirani zake wa Ghuba kujibu mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel.

Waandishi wa habari wa AFP wameripoti kusikia milipuko kadhaa mikubwa katika miji mikuu ya Qatar na Bahrain, na pia katika jiji lenye watu wengi zaidi katika Falme za Kiarabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *