Chanzo cha picha, Christoph Greztmacher
-
- Author, Jacob Boswall
- Nafasi, BBC Monitoring
-
Muda wa kusoma: Dakika 5
Wakati Marin Petrović alipowasili mjini Bamako mwezi Septemba mwaka uliopita, alikuwa mwenye furaha.
Raia huyo wa Bosnia, alikuwa ametuma maombi ya kupata kibali cha kusafiri nchini Mali ila maombi yake yalikuwa yakikataliwa kwa misingi ya ukosefu wa usalama.
Taifa hilo lililoko Afrika Magharibi limekuwa likikabiliana na vita vya wenyewe kwa wenyewe,uingiliaji wa majeshi ya kigeni na makundi yenye itikadi kali.
“Sasa Visa yangu imekubalika na nafurahia kuanza safari yangu” Aliandika kwenye ukurusa wake wa Instagram tarehe 15, mwezi Novemba 2025.
Petrović alikataa kuzungumza na BBC wakati tunaandika taarifa hii.
Mpango wake ulikuwa wa kuzuru maeneo tofauti ya kihistoria, kabla ya kurejea nyumbani kwao.
Mjini Bamako, Petrović alifurahia mandhari ikiwemo kutembelea soko,barabara za mji huo, shule na hata kunywa vileo za nchi hiyo, kulingana na machapisho yake kwenye mitandao ya kijami.
“Siku inayofuata nilielekea Mopti, inayojulikana kuwa na msikiti uliojengwa na matope miaka mia moja iiyopita.”
Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Katika mtandao wa Instagram, Petrović anajielezea kuwa “mtu anayewaokoa wanaokwea milima” na pia “anayewaongoza watu” ambaye wito wake “ishi ndoto yako”.
Ila kabla Petrović hajatimiza ndoto yake ya kuzuru Mali, ziara yake ilipata changamoto.
“Watu waliojihami waliishambulia barabara iliyopo kati ya Bla na San, anasema katika mtandao wake wa Instagram.
“Pikipiki sita zilizokuwa na magaidi wawiili, wote wakiwa wamejihami na bunduki aina ya AK-47, walizingira gari nilimokuwa ndani na kuniburuta hadi kichakani, katika eneo lisilojulikana mbali na barabara kuu…. nilikuwa nimetekwa nyara na wapiganaji wa itikadi kali wa al-Qaeda.”
Petrović alikuwa miongoni mwa wageni waliotekwa nyara katika mkumbo wa kuwalenga wageni na wataalam wa kigeni wanaofanya kazi eneo hilo la Sahel.
Hadithi yake si geni. Mwaka wa 2025, utovu wa usalama na njia mpya wanazozitumia magaidi ziliongeza visa vya utekaji nyara wa rai awa kigeni eneo la Sahel.
Takwimu kutoka Acled, shirika huru linalofuatilia vita duniani, inaonyesha kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara wa raia wa kigeni nchini Mali na Niger mwaka wa 2025, ikilinganishwa na miaka ya huko nyuma.
Kufikia mwezi Novemba mwaka uliopita, visa 30 vya watu kutekwa nyara vilikuwa vimeripotiwa , huku idadi hiyo ikihofiwa kuwa juu mwishoni mwa mwaka huo.
Kuna visa kadhaa ambavyo viliangaziwa katika vyombo vya habari vya kimataifa. Raia wawili wa falme za Kiarabu, huku mmoja aliyetekea akidhaniwa kutoka familia ya mfalme wa Emirati, nawalitekwa mwezi Septemba mwaka uliopita nchini Mali.
Sababu ya wao kuzuru taifa hilo,na jinsi walitekwa nyara bado haijulikani.
Vyombo vya habari za taifa hilo zinasema kuwa mmoja wao alikuwa akijihusisha na biashara za kuchimba dhahabu.
Raia hao kutoka familia ya Emirati hawakuzuiliwa kwa muda mrefu.Baada ya mwezi mmoja, wanaume hao walikuwa wameachiliwa baada ya fidia ya mamilioni ya dola kulipwa. Shirika la habari la Reuters linasema dolla million hamsini zilitolewa.
“Fidia ya kifalme, chanzo kikuu cha fedha kwa watekaji wa itikadi kali,Mali.” Ilisema taarifa moja ya habari iliyochapishwa Mali.
Kisa kingine kilichoaangaziwa huko Niger, ni cha raia wa Austria Eva Gretzmacher mwenye umri wa miaka 73 na rubani raia wa Marekani Kevin Rideout,ambao walikuwa wanafanya kazi ya kutoa msaada wa kibinadamu, na walitekwa walikokuwa wakiishi.
Gretzmacher, anasemekana kuwa raia wa kwanza wa umoja wa ulaya kutekwa nyara tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2023 iliyochangia kudorora kwa hali ya usalama nchini humo.
Visa vingi vya utekeaji nyara ni vya raia wa kiafrika, na idadi hiyo inajumuisha maelfu ya watu kila mwaka ikichochewa na watu kupotezwa na ugaidi, kama nchini Nigeria ambako mwaka jana ilirekodi visa vingi vya utekaji nyara.
Utafiti wa BBC aidha umebaini kuwa raia wa China ndiyo walitekwa nyara zaidi barani Afrika.
70% ya visa vya utekeji nyara barani Afrika vilitokea eneo la Sahel katika mataifa ya Mali na Niger.
Kati ya raia wakigeni 89 waliotekwa, 38 walikuwa na pasipoti ya China, huku raia wa India wakiwa 14.
Wengi wa watu hawa walikuwa wanafanya kazi nchini Mali katika eneo lililo na dhahabu la Kayes, Sikasso na Koulikoro, maeneo ambayo kampuni za China zimekuwa zikiendesha oparesheni ya uchimbaji dhahabu.
Kundi linajihusisha na kundi la kigaidi la al-Qeada, Jama’at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM), ndiyo inalaumiwa kutekeleza mashambulizi na utekaji nyara katika mataifa ya afrika magharibi ya Sahel, haswa Burkina Faso, Mali na Niger.
Kulingana na makadirio fidia inayolipwa baada ya utekaji nyara, huchangia 40% ya mapato ya kundi la JNIM kila mwaka.
Raia wa kigeni huonekana kuwa thamani kwa kundi la JNIM, kwa sababu wao huto fidia ya juu ikilinganishwa na kuwateka raia wa nchi hiyo, na pia huwapa nguvu ya kufanya majadiliano na serikali ya Mali.
Kuanzia mwezi Septemba mwaka uliopita JNIM imekuwa ikishambulia gari za mafuta zinazoelekea mjini Bamako, na kufanya mji huo kukosa bidhaa hiyo muhimu na kulemaza shughuli nyingi.
Hii ikiwa mojawapo ya njia wanazozitumia kuilemeza uchumi wa Mali na serikali ya kijeshi ya Mali iliyochukuwa madaraka mwaka wa 2020.
Lengo kuu la kundi la JNIM ni kuhakikisha inakuwa ghali sana na hatari kwa kampuni za kigeni kuwekeza nchini Mali.
Petrović alikaa zaidi ya mwezi mmoja kama mfungwa wa JNIM.
“Nililala kwenye sakafu kwa siku 55, nilikunywa maji kutoka kwa kisima ambacho wanyama wanaenda haja pale ili niweze kuishi, nilikuwa nakula wali mkavu bila chochote. Ningeamka kusikia milio ya Wanyama wa aina yote ikiwemo mbwa mwitu na fisi, na kila siku ningewaua nge iliniweze kulała.” Aliandika katika ukurusa wake tarehe 16 mwezi Novemba.
Licha ya masaibu aliyoyapitia, Petrović aliachiliwa pamoja na raia mwingine wa Bosnia mwishoni mwa mwezi Oktoba baada ya kushikiliwa kwa zaidi ya siku 50.
Aliachiliwa bila kulipa fidia yoyote.
Petrović hajachapisha maelezo yoyote ya jinsi aliachiliwa huru, ila alisema aliweza kuishi kutokana na uzoefu wake wa kukwea milima na kufanya walichokuwa wakitaka wagaidi hao.
Inasemekana kundi hilo la JNIM liliwaachilia huru raia ha owa Bosnia bila fidia ili kuwavutia mataifa ya magharibi na kuonyesha kuwa hawana nia mbaya.
Sababu nyingine inaweza kuwa kwamba China hufanya juhudi ndogo kuingilia kati au kuweka shinikizo la kidiplomasia katika matukio ambapo raia wake wametekwa nyara.
Hata hivyo, kuna baadhi ya dalili za hivi karibuni zinazoonyesha mabadiliko ya msimamo kutoka kwa serikali ya China.
Tukio moja lililoripotiwa tarehe 27 Novemba, ambapo wafanyakazi sita wa China walidaiwa kutekwa nyara, taarifa kutoka ubalozi wa China nchini Mali iliyoonya dhidi ya shughuli za uchimbaji dhahabu “haramu” nchini Mali, na kuwataka raia wa China kuufunga oparesheni zao na kuwaondoa wafanyakazi wao nchini humo.
Ubalozi wa China nchini Mali bado haujajibu ombi la kuzungumza na BBC.
Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Ila kuna wale ambao hawajakuwa na bahati kama Petrović.
Eva Greztmacher raia wa Austria mwenye umri wa miaka 74, bado ameshikiliwa mwaka mmoja baadaye baada ya kutekwa nyara.
Mwanawe kijana Christoph Gretzmacher, anahofu, hajui iwapo mama yake ambaye amezeeka kiumri anaweza kustahimili mazingira ya jagwani.
“Nyuzi joto ya hadi 50C inahatarisha maisha ya watu wengi ambao hawana uzoefu wa eneo hilo.” Aliiambia gazeti moja la Austria mwezi Januari.
Imetafsiriwa na Beldeen Waliaula