
Wanajeshi wa Marekani wameendelea kutekeleza mashambulio nchini Iran, huku Israeli nayo ikishambulia Lebanon siku ya Jumatatu, katika vita ambavyo vinendelea kusambaa kwenye nchi za Mashariki ya Kati.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Vita vya Marekani na Israeli nchini Iran, vilianza Jumamosi iliyopita na kusababosha kifo cha kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.
Marekani na Israel zinasema lengo la mashambulio hayo ni kuharibu kabisa miundo mbinu ya Iran ya kutengeneza silaha za maangamizi, lakini pia kubadilisha uongozi wa nchi hiyo.
Iran nayo imetekeleza mashambulio kulenga kambi za kijeshi za Marekani katika nchi za Mashariki ya Kati, lakini pia kulenga Israel, na kusababisha maafa ya watu kadhaa.
Shirika la taifa la Habari la Iran limesema, watu 20 wameuawa katikati ya jiji la Tehran na hospitali na jengo la polisi kuharibiwa, kufuatia mashambulio ya Marekani.
Israel nayo imewaambia wakaazi wa vijijji zaidi ya 50 nchini Lebanon, kukimbilia maeneo salama baadaya kundi ka Hezbollalh kurusha makombora katika ardhi ya Israeli.