Chanzo cha picha, Reuters
Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia imethibitisha kwamba ubalozi wa Marekani mjini Riyadh ulishambuliwa na ndege mbili zisizo na rubani, kulingana na makadirio ya awali.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, wizara hiyo ilisema hii ilisababisha “moto mdogo na uharibifu mdogo wa vifaa kwenye jengo hilo”.
Ubalozi wa Marekani umewaagiza wafanyakazi wake walioko Saudi Arabia kubaki ndani katika miji ya Jeddah, Riyadh, na Dhahran kutokana na uwezekano wa tishio la kiusalama.
Ujumbe huo utapunguza au utaepuka safari zisizo za lazima kwenda kwenye vituo vya kijeshi katika eneo hilo, kama tahadhari kwa sababu za usalama.
Donald Trump alikiambia kituo cha runinga cha NewsNation kwamba Marekani italipiza kisasi “hivi karibuni” kufuatia shambulio dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Riyadh na vifo vya wanajeshi wa Marekani.
Wanajeshi sita wa Marekani wameuawa hadi sasa huku 18 wakiwa wamejeruhiwa, Marekani ilisema Jumatatu usiku.
Unaweza kusoma;