#HABARI:Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, Dkt. Jafar Seif ameagiza kuhamishwa kwa vifaa tiba vilivyohifadhiwa au kufungwa katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya tangu mwaka 2020 lakini havitumiki mpaka sasa kwa sababu mbalimbali, na kuelekeza ama vianze kutumika au vihamishiwe katika vituo vyenye wataalamu ili vitumike kuwahudumia wahitaji.
Dkt. Seif ametoa agizo hilo wakati akizungumza na waganga wakuu wa mikoa yote Tanzania bara jijini Dodoma, katika kikao maalum kilicholenga kujadili changamoto zinazotatiza ubora wa utolewaji wa huduma za afya na kuweka mikakati madhubuti katika utekelezaji wa mpango wa bima aya afya kwa wote.
Amesema licha ya Serikali kununua vifaa tiba vya kisasa, baadhi ya vifaa hivyo imebainika bado havijaanza kutumika tangu mwaka 2020 kutokana na sababu mbalimbali na hivyo kuagiza kuwa ni vyema vikahamishiwa katika maeneo yenye wataalam na vianze kutoa hudumu kwa jamii ili kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaohitaji huduma za vifaa tiba hivyo.
“Hatua zichukuliwe haraka kuvifanya vitumike au vihamishiwe vituo vyenye uhitaji, kwani haitavumilika tena vifaa kuwepo bila kutoa huduma” alisema Dkt. Seif.
Katika hatua nyingine Dkt. Seif amesema kuanzia sasa serikali haitaruhusu kuanizhswa kwa maboma mapya ya vituo vya kutolea huduma za afya ili kutoa nafasi ya kumalizia maboma yaliyopo kwa sasa ambayo bado hayajamalizika.
“ Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ametuelekeza kuwa, lazima kwanza tumalize maboma yaliyopo ambayo ni zaidi ya 1800 kwahiyo tunajua kuna ahadi za waheshimiwa viongozi ambao ni Wabunge na Madiwani za kuanzisha maboma ili Serikali imalizie lakini kwa sasa tunajikita kwanza kumalizia haya yaliyopo,”alisema Dkt. Seif.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.