
Msemaji wa ofisi ya rais Salva Kiir amesema hii leo kwamba mamlaka zilipitiwa wakati wa uteuzi baada ya Steward Sorobia Budia, mwanasiasa wa zamani wa upinzani kuwa miongoni mwa wajumbe waliotajwa katika amri iliyotolewa na Kiir.
Budia alifariki miaka mitano iliyopita.
Taarifa zinasema familia ya marehemu sasa inadai fidia, kwa kuzingatia tamaduni zinazokataza kuomba au ‘kuamsha’ roho ya marehemu bila ufahamu, ridhaa au ushiriki wa familia.
Hakujawahi kufanyika uchaguzi nchini Sudan Kusini iliyopata uhuru tangu 2011, na ambayo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kila mara.