1. MONUSCO yaishukuru Afrika Kusini baada ya kutangaza uamuzi wake wa kuondoa wanajeshi wake DRC

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, (MONUSCO) umetoa taarifa kwamba umefahamishwa na Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa kuwa Afrika Kusini itaondoa vikosi na wanajeshi wake waliobaki ndani ya MONUSCO

Katika taarifa iliyotolewa jana kutoka ofisi za MONUSCO kwenye mji mkuu wa DRC, Kinshasa, MONUSCO inaeleza shukrani zake za dhati kwa Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Afrika Kusini kwa kujitolea kwao kwa dhati kwa kipindi cha miongo kadhaa katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, pamoja na kwa kujituma kwa walinda amani wa Afrika Kusini katika kuunga mkono utekelezaji wa jukumu la Ujumbe huu wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini DRC.

MONUSCO pia katika taarifa hiyo kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa inatoa heshima kwa walinda amani wa Afrika Kusini waliopoteza waliofariki dunia wakihudumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa katika huduma ya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na inaheshimu kujitolea maisha yao.

Pamoja na Afrika Kusini kutangaza hivyo kuwa itaondoa wanajeshi wake DRC, MONUSCO inaeleza kwamba inatarajia kuendelea kushirikiana na Jamhuri ya Afrika Kusini katika masuala mapana ya ulinzi wa amani, ikiwemo kujifunza kutokana na uzoefu uliopatikana na kuendelea kuunga mkono juhudi zinazolenga kuimarisha amani na utulivu.

“MONUSCO itafanya kazi kwa karibu na Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa pamoja na wadau husika ili kuhakikisha kuwa mpito wowote unaohusiana na uamuzi huu unasimamiwa kwa njia salama, yenye utaratibu na uwajibikaji, kwa kuzingatia viwango na mahitaji ya kiutendaji ya Umoja wa Mataifa,” inaeleza taarifa hiyo.

Taarifa rasmi za serikali ya Afrika Kusini zinaeleza kuwa nchi hiyo ni miongoni mwa nchi kumi za juu zinazochangia wanajeshi wengi zaidi kwa MONUSCO, ikiwa na zaidi ya wanajeshi mia saba waliotumwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ili kuunga mkono jukumu la MONUSCO la kulinda amani nchini DRC.

Mwanamke katika Navy bluu polo shati na kola nyeupe ana smartphone na nyeupe earphones plugged katika. Yeye ni kuzungumza, pengine wakati wa mahojiano au uwasilishaji. Katika background, mtu amevaa miwani ni kuonyeshwa katika picha ndogo inset, kurekebisha miwani yake.

Hai Anh, mwanafunzi wa Chuo Kikuu Hanoi kilichoko Hanoi, mji mkuu wa Vietnam, ambaye ana ulemavu wa kutoona.

2. Msichana mwenye ulemavu wa kuona asema, “tuwekeeni mazingira sahihi ili nasi tuoneshe uwezo wetu”

Nchini Vietnam taifa lililoko kusini-mashariki mwa Asia, mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu mwenye ulemavu wa kutoona anajitahidi kuhakikisha anatimiza ndoto yake ya kuwa mtaalamu wa mawasiliano licha ya vikwazo anavyokumbana navyo kila uchao, na hii ni kwa sababu si kwamba njia ni rahisi bali kwa sababu dhamira yake ni kubwa zaidi. 

Video inaanzia kwenye Chuo Kikuu Hanoi kilichoko Hanoi, mji mkuu wa Vietnam, mwanachuo Hai Anh akishuka ngazi kwa kutumia fimbo yake inayomwongoza.Anasema nataka kusaka njia yangu mwenyewe lakini kuna vikwazo vingi ambavyo lazima tukabiliane navyo. Mathalani kuna gharama za ziada ambazo tunalazimika kukabiliana nazo.

 Hai akiwa ndani ya moja ya madarasa anasema ana umri wa miaka 25 na yuko mwaka wa tatu Chuo Kikuu akijikita katika Mawasiliano ya Umma katika Shule ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma.

Ingawa haoni, Hai anatumia simu yake janja yenye apu zinazomwezesha kusoma kupitia nukta nundu.

“Nadhani moja ya changamoto kubwa na vikwazo wanavyokabiliana nazo watu wenye ulemavu na watu wenye ulemavu wa kutoona kama mimi ni ubaguzi kutoka kwa waajiri. Halikadhalika kutoka kwa wenzangu walionizunguka.”

Kando ya gharama ya ubaguzi ni gharama za nyenzo za kumrahisishia maisha yake.

Vile vile lazima nilipie gharama ya teknolojia nyingine kama apu ya Joy Screen ambayo naitumia kwa ajili ya kusoma kwenye simu. Gharama ya laptop mahsusi na fimbo nyeupe.”

Vietnam hupatia posho familia zenye watoto wenye ulemavu na Hai anasema hutumia posho hiyo kulipia gharama za ziada.

Akiwa kwenye ukumbi akicheza dansi na kisha anachukua mikrofoni na kuimba Hai anasema…

“Ili kukabiliana na ubaguzi kutoka kwa wale wanaotuzunguka, kwanza lazima sisi wenyewe tuondoe vikwazo tulivyojiwekea wenyewe. Kwanza ni kuimarisha na kuendeleza uwezo wetu. Na kwa vikwazo vya kijamii naamini serikali, mashirika na sekta binafsi wataungana na kuweka mazingira ya kuajiri watu wenye ulemavu ili kuonesha uwezo wetu na kukidhi mahitaji yetu.”  

Umoja wa Mataifa unasema asilimia 15 ya wakazi wa dunia wana ulemavu sawa na watu bilioni 1 ambapo kati yao hao asilimia 80 wako kwenye umri wa kufanya kazi, hivyo ujumuishi ni suala lisilo na mjadala.

Mwanamke katika hijab ya manjano akizungumza kupitia kipaza sauti kwa kundi la wanafunzi walioketi kwenye viti katika sherehe ya shule ya nje huko Tana River, Kenya, kama sehemu ya Mpango wa Jamii Nzuri.

Mwanaharakati wa wanawake kuhusu Ukeketaji au FGM anazungumza katika hafla ya elimu kwa jamii huko Tana River, Kenya.

3. Nilirubunika nikadhani ukeketaji ni usafi kumbe ni jinamizi: Manusura Saadia Hussein

Ukeketaji au FGM ni jinamizi linalowaandama waathirika maisha yao yote likisababisha changamoto sio tu za kimwili lakini pia za kiafya na kuwaacha na makovu yasiyofutika. Katika Kaunti ya Tana River Kusini Mashariki mwa Kenya tunakutana na manusura na shujaa mwanaharakati wa kupambana na mila hiyo potofu ya ukeketaji Saadia Hussein, raia wa Somalia anayeishi Kenya hivi sasa. Mkurugenzi mtendaji na mwanzilishi wa taasisi  isiyo ya kiserikali ya Brighter Society Initiative anasimulia safari yake ya machungu ya ukeketaji akisema, 

“Nilikeketwa nikiwa mdogo wa umri wa miaka 10 na wakati huo nilikuwa na furaha sana nikijisi na mimi nitakuwa kama wasichana wengine, kwa sababu kulikuwa na unyanyapaa shuleni na mara nyingi nlikuwa nalia wakati wasicha wengine walipokuwa wananisema vibaya, wanasema mimi ni mchafu. Hivyo nilikuwa nampa mama yangu shinikizo nami nifanyike , kwa sababu akiliyangu ilikuwa inafikiria huu uchafu ni kusafishwa tu, akili yangu ilikuwa na taswira tofauti kabisa.”

Na je alipowasili kwa ngariba mambo yalikuwaje?

“Siku ya kukeketwa nilijuta hiyo siku nilipelekwa msituni na nikajiuliza mbona napelekwa msituni na ni kuoshwa tu msituni tunaenda kufanya nini? Lakini nikanyamaza , mara nikaona kina mama wanakuja na aliyenikeketa alikuwa nyanya yangu mzaa baba. Sasa hapo nikapata mshtuko. Nikitaka kuuliza maswali hakuna wa kumuuliza. Nikawekwa chini na wamama wakanishikilia mikono , wengine wananiziba mdomo kwa nguo siwezi piga kelele. Nyanya akachukua kiwembe hiyo ilinishangaza sana nivyotarajia na kilichofanyika ni tofauti kubwa.”

Saadia anasema wasicha wengi hutumbukia kwenye ukeketaji sababu hawajui watakachokutana nacho 

“Baada ya kupona na kurudi shuleni wale wasichana hawakuwa rafiki zangu tena kwa sababu nilijua na kuamini kuwa wao ndio walinisukuma niweze kufanyiwa ukeketaji na hawakuniambia ni nini kinanisubiri na wasichana wengi mara nyingi wanakimbilia ukeketaji kwa sababu hawajui ni nini kinawasubiri huko. Na hiyo ndio Bahati mbaya kwa sababu hakuna mtu anayekuelezea haswa nini nini kinafanyika kwa ukeketaji.”

 Na nini hasa kilimsukuma Saadia kuingia kwenye uanaharakati?

“Baada ya kuolewa kila mtu huwa anatarajia mtoto, sasa hapo ndipo nilipoanza kuwa mwanaharakati, kivipi? Nilikuwa kwa uchungu wa uzazi kwa siku tatu siwezi kujifungua , wakunga wanakuja na unakatwa kila mahali bila mpangilio bora mtoto atoke hawajali utakuwaje. Na baada ya siku tatu ndio nikajifungua na nikapoteza fahamu hata sikujua nini kinaendelea..(..jump to 0.10:04-0.10:15) Hapo ndio nikazidi kuongeza juhudi  na kusema kwamba ukeketaji madhara yake hayaishii tu unapokatwa yamenifuata maisha yangu yote.”

Ili kujua zaidi kile anachokifanya sasa Saadia kupambana na jinamizi hilo la ukeketaji usikose kujiunga nasi katika sehemu ya pili ya simulizi yake kwenye vipindi vyetu vijavyo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *