#HABARI: Kiza Mayeye, aliyeteuliwa na chama cha Allaince for Change and Transparent, (ACT-Wazalendo) kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini, amefika katika ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo na kukabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa kwa wananchi ili kuwatumikia kwa nafasi hiyo.
Akizungumza baada ya kumkabidhi fomu, Linus Skainda, Msimamizi wa uchaguzi amesema uchaguzi inaongozwa na sheria na kanuni na hivyo haki itatendeka na kuonekana.
Amesema mpaka sasa wamejitokeza wagombea ubunge kutoka vyama 11 waliochukua fomu za kugombea nafasi ya ubunge ikiwemo chama cha NRA, UDP, TLP, AFP, NLD, CUF, ADC, ADA, THADEA,CCM, na ACT.
Akiongea na wananchi mara baada ya kuchukua fomu hizo na amesema amejitoa kuwapigania watu wa Kigoma Kaskazini, kwa kuwa na yeye ni mtoto wa jimbo hilo na kwamba yupo tayari kutumia kile alichopewa na Mungu kwa ajili ya ustawi wa watu wa jimbo hilo.
Miongoni mwa vipaumbele vyake endapo atapata ridhaa ya kuwa mbunge ni pamoja na kutatua changamoto za huduma bora za Afya akilenga kuondoa utofauti wa matibabu kati ya matajiri na masikini, kupambana kwa ajili ya elimu bora pamoja na kuondoa umaskini kwa wananchi ili wawe na uhakika wa milo mitatu kwa siku.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania