Maafisa watatu wa polisi wameuawa na wengine saba kutekwa nyara jana Jumapili katika shambulio la wanamgambo wenye silaha katika Jimbo la Benue nchini Nigeria.

Benjamin Hundeyin Afisa Mahusiano ya Umma wa Polisi ya Nigeria ameeleza kuwa watu wenye silaha wasiojulikana waliwazia na kuwashambulia polisi kwa silaha katika eneo la Agu katika jimbo la Benua. Hundeyin amesema kuwa  maafisa watatu wa polisi wameuawa na wengine saba wametekwa nyara wakati wa shambulizi hilo. 

Ameongeza kuwa: askari usalama tayari wametumwa katika jimbo la Benue na hadi sasa wamewatia mbaroni washukiwa sita kufuatia tukio hilo.  

Katika miaka ya karibuni Nigeria imeathiriwa na wimbi la mashambulizi katika maneo mbalimbali ya nchi hiyo yanayotekelezwa na megenge yanayobeba silaha pamoja na makundi ya kigaidi yakiwemo kundi la kigaidi la Boko Haram na tawi la magharibi mwa Afrika la kundi la ISIS (Daesh). 

Makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha mara kwa mara huwateka watu nyara mkabala wa kupatiwa mlungura licha ya adhabu ya kifo iliyoainishwa na nchi hiyo kwa yoyote atakayepatikana na hatia ya jinai kama hizo. 

Makundi hayo yenye silaha mara nyingi huvamia vijiji, skuli na wasafiri khususan katika majimbo ya kaskazini mwa Nigeria na kudai kupatiwa fedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *