
Dar es Salaam. ‘Long taimu’ maisha yalikuwa mchekea na watu walishikana. ‘Of coz’ kipato kilikuwa kidogo sana lakini walikuwa na familia kubwa. Watoto kibao, wake kibao, ‘smolo hausi’ na kulea watoto wa ndugu kibao humo humo.
Pamoja na hayo, watu walimudu majukumu ‘kozi’ mishe za ‘laifu’ pindi hicho zilikuwa ‘ize’ kinyama. Na pia malezi lilikuwa jukumu la ukoo mzima, mtoto hakulelewa na wazazi wake peke yao. Wengi wetu tumekulia kwa wajomba na mashangazi.
Leo hali imebadilika, elimu, afya, makazi na bata batani vinahitaji pesa kibao. Wengi wanaona bora kuzaa watoto wachache, malezi bora na fursa nzuri. Kuliko rundo la watoto na kutegemea kudra za Mungu kwa msosi na ‘ishu’ ya ‘dei tu dei’.
Hata mademu wengi leo waajiriwa ama wafanyabiashara. Hawana ‘taim’ ya kulea na kuvalishana zile pampasi. So! Suala la kupanga uzazi na ukubwa wa familia, ni suala la kuangalia uchumi na muda zaidi, badala ya mila zetu na macho ya walimwengu.
Mazingira ‘yamechenji’ siyo tu kitabia nchi, hata kitabia watu. Kitambo hicho wakati tunakua sisi, tulikwiba mayai ‘homu’ ili tukahonge totozi. Leo madogo wanapiga kizinga kwa pisi zao hata pesa ya kusuka mkeka ili amlize mdosi.
Unajua nini? Jua limekuwa kali sana mfukoni, mpaka linaondoa ubora wa kiumeni kwa madogo. Ndo maana ndoa za leo ni shida tupu, madogo wamepigwa ganzi. Hata vumbi la Kongo halina tena nguvu. Bongo zao hazina pozi la kiumeni kabisa.
Tendo la ngono linahusisha akili yako kwanza. Ukiwa na ubongo tengefu, jipake mavumbi yako na maombezi ya Mwamposa juu. Ni kazi bure, havisaidii kitu. Madogo siyo tu hawawezi kuwalea watoto, hata tumbo lililomleta duniani (mama mzazi).
Wazee walikuwa na wake wengi, wakawa na michepuko kibao. Na zaidi walilea na watoto wa ndugu na maisha yakawa poa tu. Leo hii mtoto mmoja huachwa akalelewe na mamaake. Madem wana fursa nyingi za kipato kuliko masela. Tehe! tehe! tehe!
Hapa ndo inakuja tofauti ya Baba, Dingi, Faza na Mshua. Ni majina yenye maana ya mzazi wa kiume. Lakini madogo hutumia kulingana na ‘laifu staili’ ya mzee. Hili hata kwa mabraza na maanko lipo pia, huitwa kutegemea na sifa zako. Anko na mjomba ni tofauti.
BABA;
Ni mzazi wake wa kiume ambaye anatimiza wajibu. Anayeishi kwa kufuata miiko ya mzazi wa kiume. Huwajibika kwa watoto na familia ipasavyo, hata kama kipato chake cha chini. Yaani ni mtu anayeishi kulingana na role yake. Huyu ndo Baba.
DINGI;
Kile alichoimba Domokaya, ndo mulemule. Siku zote madingi ni miyeyusho sana, siyo tu kukimbia familia. Hata kama yupo home na anawajibika, lakini ana mikasa ya kidwanzi. Mtu wa mitungi labda, au madem na hajijali. Huyo ndo dingi.
FAZA;
Ndo wale wazee wanaenda sawa na watoto wake. Yaani ‘anashoo lavu’ kwa watoto, lakini ‘samtaim’ kwa ‘Bi mkubwa’ wao anazingua kinoma. Nje ya nyumba utaona ni mtu mwema lakini ‘insaidi’ ajabu halali chumba kimoja na mkewe. Huyo ndo ‘Faza’.
DADII;
Hawa ndo wale mabraza flan hivi wamekata ringi. Alisoma vizuri tu na anajipenda sana, na viingereza vyake vya Azania Sekondari ama Kigurunyembe kama siyo Iyunga Tech. Ila anategemea mishe za mkewe ili familia iishi. Huyu ndo Dadii.
MSHUA;
Ndo wale wanaondoka na kurudi usiku bila kuonana na watoto. Atasafiri nje na kurudi anayejua ni mkewe na ofisini kwake. Familia inaishi maisha mazuri kwa msosi na kila kitu, ila ukaribu na watoto kwake ni sifuri. Huyu ndo Mshua.
Kwa nyongeza tu, kuna wale wa kuitwa Mzee. Hawa huwa wakali sana kwa watoto na wake zao. Wengi wana mali zisizohamishika kama nyumba, mashamba na hupenda kuhangaika na mambo ya kanisani au jumuiya hizi. Ndo wanaitwa Mzee.
Na haya majina huanzia ujanani kitabia. Tabia za kupuuzia puuzia vitu, mwisho uzeeni utaitwa Dingi. Hata uwe na elimu na pesa nyingi bado utaitwa dingi. Kwa sababu suala la kupuuzia vitu ni tabia na siyo mafanikio. Wewe ni dingi tu wala siyo poa.
Ndivyo ilivyo kwa Faza, Mshua, Baba na Dadii. Ni wewe kuamua leo ujanani unataka utambulike kwa jina lipi uzeeni mwako. Na tuweke sawa, uzee hauna miaka mingi ni hivi punde tu utakuwa mzee. Uzee ni baada ya kushea mbegu na mwanamke.
Hata kama una miaka chini ya arobaini. Kama una watoto wewe ni mzee tu. Utakuwa na viungo na ngozi ya ujana ila utambulisho ni wa kizee. Watoto wana wenzao wanaowapa habari za mzee wao ambaye ni wewe. Badilika sasa siafu wewe.
Sasa endelea kuishi ‘laifu’ lako la kindezi ndezi, uzeeni uwe bwege bwege. Wazee wetu hawakuwa mapimbi, ndo maana na sisi siyo mapimbi. Lakini madogo wa sasa mmekaa kiwaki sana, kiasi cha kuchagua dem kwa kutumia akili mnemba.
Acheni upoyoyo.