Pakistan imesema, makubaliano ya hivi karibuni ya kiulinzi ambayo hayajawahi kushuhudiwa iliyosaini na Saudi Arabia yanalingana na yale yaliyopo katika Muungano wa kijeshi wa Magharibi wa nchi wanachama wa NATO.

“Ni aina ya kama ilivyo [mikataba] mingine mingi ya kujihami; na nadhani njia bora ya kuiangalia ni kuangalia (kwa kuifananisha na) NATO,” ameeleza msemaji wa serikali ya Pakistan Musadik Malik katika mahojiano aliyofanyiwa jana Jumamosi na televisheni inayomilikiwa na serikali ya Saudia ya Al Arabiya. 

Riyadh na Islamabad zilitia saini siku ya Jumatano iliyopita huko mjini Riyadh, Saudi Arabia “Mkataba wa Kiulinzi wa Kimkakati wa Pande Mbili” wakati wa mkutano kati ya Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif na Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman, ambapo pande hizo mbili zimeuita mkataba huo “mkataba wa kimkakati wa aina yake.”

Mkataba huo unakichukulia kitendo chochote cha uchokozi dhidi ya nchi moja kuwa ni sawa na kuzishambulia nchi zote mbili na hivyo kukabiliwa na ulipizaji kisasi wa pamoja wa Islamabad na Riyadh.

Katika uchambuzi iliofanya kuhusiana na kipengele hicho kufuatia kusainiwa mkataba huo, gazeti la Business Recorder la Pakistan limeandika: kulingana na makubaliano hayo, “uchokozi wowote dhidi ya Pakistan au Saudi Arabia utachukuliwa kama uchokozi dhidi ya mataifa yote mawili.” Na kwa msingi huo, kitendo kama hicho cha kichokozi “kitaongeza uwezo wa pamoja wa kuzuia (hujuma)”…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *