Akikosoa misimamo dhaifu ya nchi za Kiarabu na Kiislamu katika kikao cha hivi karibuni cha Doha dhidi ya hujuma ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Qatar, kiongozi wa Ansarullah amesisitiza kuwa, vitisho vya Israel haviko kwenye medani ya Palestina pekee bali vinalenga jamii nzima ya Kiislamu.

Sayyed Abdul Malik Al-Houthi, kiongozi wa Ansarullah amesisitiza katika hotuba yake ya jana juu ya kuendelea uungaji mkono wa pande zote wa watu wa Yemen na vikosi vya kijeshi kwa ajili ya watu wanaodhulumiwa wa Gaza na muqawama wao wa kijasiri.

Al Houthi ameendelea kuashiria jinai za kivita na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza na kusema kuwa, utawala ghasibu wa Israel unaendeleza jinai hizo za karne katika Ukanda wa Gaza mbele ya macho ya walimwengu wote.

Akiashiria utawala wa Kizayuni unavyotumia vibaya udhaifu na mgawanyiko wa nchi za Kiarabu na Kiislamu na misimamo yao dhaifu, kiongozi wa Ansarullah amesisitiza kuwa, vitisho vya Israel haviko kwenye medani ya Palestina pekee bali vinalenga mataifa yote ya Kiislamu.

Al-Houthi amesema kuwa matukio ya kutisha na maafa ya mauaji ya halaiki yanalazimisha mtu yeyote aliye na dhamiri ya kibinadamu kuchukua msimamo.

Aliendelea kusema, “Waislamu ni watazamaji na wamewaacha watu ambao wao ni sehemu yao (yaani watu wa Palestina huko Gaza) peke yao, huku Waislamu wote wakikabiliwa na njama na mipango ya Wazayuni.”

Kiongozi wa Ansarullah ya Yemen amefafanua kuwa silaha ya muqawama ni ngao ya usalama na ngome imara ya kuunga mkono mataifa na kuyazuia na kuyaweka mbali na mauaji ya kimbari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *