Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, maambukizi 48 ya ugonjwa wa Ebola yamethibitishwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na watu 31 wamefariki dunia.

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus amewaambia waandishi wa habari kupitia video kutoka makao makuu ya WHO mjini Geneva Uuswisi kwamba: “Imepita wiki mbili tangu serikali ya DRC itangaze mlipuko wa Ebola …Hadi sasa, maambukizi 48 yamethibitishwa…, na watu 31 wameaga dunia,”.

Mlipuko huo, wa kwanza nchini humo katika kipindi cha miaka mitatu, ulitangazwa mapema Septemba.

Shirika la Afya Duniani Jumapili lilisema limeanza kutoa chanjo kwa wafanyikazi wa afya walio mstari wa mbele na walio wasiliana na watu walioambukizwa virusi vya Ebola katika Mkoa wa Kasai nchini Congo, ambapo mlipuko umetangazwa.

WHO imesema dozi 400 za awali za chanjo ya Ervebo Ebola kutoka akiba ya dozi 2,000 nchini humo zimefikishwa Bulape, kitovu cha mlipuko huo.

Mara ya mwisho kwa maambukizo hayo kuripotiwa nchini DRC, ilikuwa miaka mitatu iliyopita ambapo watu 6 waliripotiwa kufariki. Jamhuuriy a Kidemokrasia ya Congo ikiwa na historia ya kusumbuliwa milipuko ya Ebola tangu mwaka 1976, ila kati ya mwaka 2018 hadi mwaka 2020 ndipo nchi hiyo imeshuhudia kipindi kirefu cha mlipuko wa ugonjwa huo zaidi ya watu 2, 300 wakiripotiwa kufa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *