Shirika la Msamaha Duniani, Amnesty International, limekosoa vikali kura ya turufu ya Marekani dhidi ya azimio la kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, likitaja hatua hiyo kama uungaji mkono wa moja kwa moja kwa jinai za kutisha za Israel.

Limeichukulia kura ya turufu ya Marekani dhidi ya azimio la usitishaji vita huko Gaza kuwa ni kuunga mkono kuendelea jinai za utawala ghasibu wa Israel na kusema: ‘Badala ya kutumia ushawishi wake kuzima maafa ya kibinadamu, Marekani kwa mara nyingine tena imetumia vibaya kura yake ya turufu na hivyo kuruhusu kuendelea mauaji ya kimbari ya Israel katika Ukanda wa Gaza.’

Matokeo ya kura hii ya turufu ni mabaya kwa watu wa Gaza; ambapo mashambulizi ya Israel yamepelekea mamia kwa maelfu ya watu kukimbia na kurundikana katika maeneo yasiyo salama na hivyo kuendeshwa kampeni ya mauaji ya kimbari ambayo hayajawahi kushuhudiwa tena katika eneo. Amnesty International imeikosoa vikali Washington na kusema: ‘Marekani, kwa kutojali kwake, imesimama peke yake mbele ya jamii ya kimataifa kwa kuihimiza Israel kuendeleza mauaji ya kimbari; Kitendo ambacho historia haitakisamehe hata kidogo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *